// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); JUVE BINGWA WA DROO ITALIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE JUVE BINGWA WA DROO ITALIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 08, 2012

    JUVE BINGWA WA DROO ITALIA


    KLABU ya Juventus ilipoteza nafasi ya kulingana kwa pointi na AC Milan Jumatano baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Bologna.
    Nahodha wa Bologna, mwenye umri wa miaka 35, Marco Di Vaio aliwafungia bao la kuongoza wenyeji dakika ya 17 na Mirko Vucinic akaisawazisha Juve dakika ya 58.
    Mechi hiyo iliahirishwa kutoka wiki iliyopita kutokana na hali ya barafu na sasa Milan inaiacha Juve kwa pointi mbili, timu zote zikiwa zimecheza mechi sawa.
    Habari mbaya kwa Juve ni kwamba, beki wake Leonardo Bonucci alilimwa kadi ya pili ya njano dakika ya 84 na kukiacha Kibibi Kizee cha Turin kiende Genoa bila mabeki wake watatu Jumapili kuwavaa wenyeji wao hao.
    Kocha anayeinoa Juventus katika mwaka wake wa kwanza, Antonio Conte pia alilimwa kadi nyekundu kiama kinga dakika ya 72.
    Juventus inabakia kuwa pekee ambayo haijafungwa katika ligi ya Itali, lakini ndio pia iliyotoa droo nyingi—13— na imeshinda mechi moja tu katika ya sita zilizopita. Juve pia ilitoka 1-1 na Chievo Verona wi9ki iliyopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JUVE BINGWA WA DROO ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top