Oboya peke yake alishangilia ushindi Slovakia |
WANASOKA wa Kenya wanaocheza nje, hawakuwa na wikiendi nzuri
kwa Victor Wanyama kupata kadi nyekundu ya kwanza tangu ajiunge na Celtic katika
Ligi Kuu ya Scotland, wakati Auxerre imeangukia kwenye shimo.
Bongostaz imepitiapitia matokeo ya klabu za Wakenya juu na
inakushushia kama ifuatavyo.
Scotland:
Celtic ilipigwa 3-2 na wapinzani wao wa jadi, Rangers sambamba
na kupoteza wachezaji watatu kwa kadi nyekundu katika mechi kali na ya kibabe. Victor Wanyama alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na kuiacha Celtic na wachezaji tisa.
Ufaransa:
Timu ya Dennis Oliech, Auxerre imebaki kwenye hatari ya
kushuka daraja baada ya kufungwa 1-0 na Toulouse, lakini mshambuliaji huyo wa
Harambee Stars aliikosa mechi hiyo kwa sababu alikuwa anatumikia adhabu ya kadi
tano za njano. Auxerre inashika mkia kwenye Ligi Kuu Ufaransa, ingawa Oliech amefunga mabao tisa msimu huu.
Italia:
Timu ya Macdonald Mariga, Parma ilitoka 2-2 na Cesena,
ingawa Mariga hakucheza kwa sababu alikuwa majeruhi baada ya kuumia kwenye
mechi na AC Milan wiki iliyopita.
Slovakia:
Mshambuliaji Patrick Oboya amekuwa kwenye kiwango kizuri na
kuiwezesha timu yake, Rozoomerok kushinda 5-2 dhidi ya Zlate katika mechi tamu,
ambayo Oboya alicheza kwa dakika 75.
DRC:
Kiungo mkongwe wa Kenya, Titus Mulama naye alikuwa kwenye
majonzi baada ya timu yake, St. Eloi Lupopo kufungwa 4-2 na Black Leopards mjini
Lumbumbashi.
0 comments:
Post a Comment