Mustafa Hoza akiwa ofisini kwake Kilombero mkoani Morogoro |
Hoza aliyekuwapo kwenye kikosi cha Simba kilichofika fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, alisema wachezaji wa Simba wanatakiwa kujua kwamba hadi sasa wamecheza dakika 45 tu dhidi ya Setif na dakika 45 nyingine watacheza Algeria.
Amewataka wachezaji wa Simba kutuliza akili na kuelekeza nguvu kwenye mchezo wa marudiano wiki mbili baadaye kwenye Uwanja wa nyasi bandia, Mei 8, mjini Stif uliofunguliwa mwaka 1972 na kukarabatiwa mwaka 2008, ukiwa na uwezo wa kumeza watu 25,000 tu.
Mabao ya Simba jana yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emanuel Arnold Okwi na kiungo Mtanzania, Haruna Moshi Shaaban ‘Boban ndani ya dakika kipindi cha pili (79 na 80).
Setif waliponzwa na mchezo wa kujihami, waliotumia muda mrefu wa mechi hiyo kabla ya kufungwa.
Kwa matokeo hayo, Simba sasa inahitaji hata sare katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo na Setif inakuwa timu ya tatu kihistoria kumenyana na Simba SC, baada ya awali Wekundu hao wa Msimbazi kutolewa na JET katika Klabu Bingwa Afrika, kabla ba wao kuitoa Al harrach katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa ujumla Simba ni mabalozi wazuri wa Tanzania katika michuano ya Afrika na wamekuwa wakifanya vema kila wanapomenyana na timu kutoka Kaskazini mwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment