ZIKIWA zimebaki siku 100 kuelekea Fainali za Kombe la
Mataifa ya Ulaya, Italia imefungwa na Marekani kwa mara ya kwanza ndani ya mechi
11 zaidi ya miaka 78, wakati Hispania, Ufaransa na Uholanzi wanaendelea vizuri
baada ya kupata ushindi mnono.
Clint Dempsey alipiga bao katika dakika ya 55 Genoa na Wamarekani
wakaibuka na ushindi wa 1-0 Jumatano usiku.
Roberto Soldado alipiga mabao matatu peke yake wakati
mabingwa wa Ulaya, Hispania wanashinda 5-0 dhidi ya Venezuela mjini Malaga. Ufaransa
iliendeleza rekodi yake ya kutofungwa katika mechi 18 wakati Oliver Giroud na
Florent Malouda walitupia nyavuni katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Ujerumani mjini
Bremen.
Uholanzi ilishinda 3-2 dhidi ya England wakati Arjen Robben akifunga
bao lake la pili dakika ya mwisho. Hicho ni kipigo cha kwanza kwa kocha Stuart
Pearce katika mechi ya kwanza akiwa kazini.
Lionel Messi alifunga hat trick hyake ya kwanza na
kuiwezesha Argentina kuifunga Uswisi 3-1.
Saudi Arabia ilitolewa katioka mechi za kuwania kufuzu
kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 kwa kufungwa mabao 4-2 na Australia, wakati
Korea Kusini, Lebanon, Oman na Qatar zimetinga raundi ya mwisho ya mchujo.
Katika mchezo mwingine baadaye sana, Colombia iliifunga Mexico
2-0 mjini Miami na Chile ilitoka sare ya 1-1 na Ghana mjini Chester, Pa.
Estonia iliifunga El Salvador 2-0 mjini Los Angeles katika
mchezo ambao refa aliumaliza baada ya dakika 89 baada ya mashabiki kuwatupia vitu
marefa wenzake.
Makocha wengi Ulaya wako chini ya jakamoyo kuelekea fainali
za Ulaya zinazoandaliwa kwa pamoja na Poland na Ukraine, ambazo zitaanza Juni 8.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew akiwa miongoni mwao, anafanya
kazai kubwa ya kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia kuelekea michuano hiyo.
Lakini Ufaransa inaweza kuwa na matumaini japo bila ya
wachezaji wake kadhaa tegemeo kutokana na ushindi wao.
Les Bleus walionyesha soka ya nguvu katika mechi hiyo na Giroud,
anayeongoza kwa mabao kwenyen ligi ya Ufaransa, aliwafungia wageni bao la
kuongoza dakiika ya 21.
Malouda alipiga la pili dakika ya 69 kabla ya Cacau kuifungia
Ujerumani la kufutia machozi dakika za majeruhi.
Ufaransa ambayo ililazimika kucheza mechi maalum ya kuwania
kiufuzu Euro ya mwaka huu, haijafungwa tangu ifungwe 1-0 na Belarus Septemba 3,
2010.
Ikicheza bila ya mfungaji wake bora, David Villa ambaye ni
majeruhi na mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres aliyetwam kikosini
Hispania kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano, mshambuliaji wa Valencia,
Soldado alichezea kwa mara ya kwanza timu ya taifa ndani ya miaka mine na
kufunga mabao matatu, kabla kocha Vicente del Bosque kuchagua kikosi chake cha
kwenda nacho kutetea Kombe.
Cesc Fabregas aliwatengenezea mabao Andres Iniesta na David
Silva kabla ya mapumziko na Soldado akapiga matatu. Hispania imeshinda mechi
zake zote nne dhidi ya Venezuela.
England ilionekana kukaribia kupata sare dhidi ya Uholanzi kwa
Gary Cahill kufunga dakika ya 85 na Ashley Young dakika ya 90, lakini Arjen
Robben alifunga bao lake la pili dakika ya mwisho na kuzima ndoto za sare kwa Three Lions.
Ireland ilipata sare ya 1-1 na Jamhuri ya Czech Republic,
ambao pia wamefuzu, wakati Simon Cox alipofunga zikiwa zimesali9a dakika nne.
Milan Baros aliwafungia bao la kuongoza Czech dakika ya 50.
Poland na Ureno zilitoka 0-0 katika mechyi ya kwanza
kuchezwa kwenye Uwanja wa taifa, mchezo utakaobeba mechi ya ufunguzi ya Euro.
Ukraine ilishinda 3-2 dhidi ya Israel.
Sweden ilishinda 3-1 dhidi ya Croatia, Ugiriki ilitoka 1-1 na
Ubelgiji na Urusi ilishinda 2-0 dhidi ya Denmark.
Wales ilifungwa 1-0 na Costa Rica mjini Cardiff, mchezo ambao
wenyeji walikuwa na matumaini ya kushinda kumuenzi aliyekuwa kocha wao, Gary
Speed.
0 comments:
Post a Comment