MAANDALIZI kwa ajili ya bonanza la vyombo mbalimbali vya
habari litakalofanyika Machi 24 mwaka huu ukumbi wa Msasani Beach Club, Dar es
Salaam yanaendelea vizuri.
George John, Mwenyekiti wa Kama ti ya Maandalizi ya Bonanza,
amesema tayari Kamati ya Maandalizi imeshatuma barua za mialiko kwa vyombo
mbalimbali vya habari na naomba wote walialikwa wathibitishe haraka
iwezekanavyo ushiriki wao kulingana na walivyojulishwa.
Pia Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA), imeshafanya maandalizi ya burudani mbalimbali kwa
ajili ya bonanza hilo, ikiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, ambao bado
tunaendelea na mazungumzo nao.
Tayari kamati imeshamalizana na bendi ya FM Academia ‘Wazee
wa Ngwasuma’ kutumbuiza kwenye bonanza hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL).
Hivyo burudani itakuwa Wazee wa Ngwasuma na wasanii wa muziki
wa kizazi kipya, ambao tutawatambulisha siku yoyote wiki hii kabla ya Alhamisi
pamoja na mgeni rasmi.
Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia
burudani, michezo na mambo mengine yawe ya aina yake.
Bonanza litaanza saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku,
ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu,
mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na
michezo.
Tunaonya kuwa kampuni ambayo itashindwa kuthibitisha ushiriki
wake mapema kwa michezo itakayocheza haitapangwa, hivyo tunaomba wahusika
watilie mkazo jambo hilo.
0 comments:
Post a Comment