// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HASIRA ZA MAN UTD, MAN CITY LIGI KUU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HASIRA ZA MAN UTD, MAN CITY LIGI KUU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 10, 2012

    HASIRA ZA MAN UTD, MAN CITY LIGI KUU ENGLAND


    Rooney wa Man Utd
    Van Persie wa Arsenal
    Gerard wa Liverpool anarudi kazini
    Dzeko wa Man City

    BAADA ya kupunguza deni la pointi katika mbio za farasi wawili za kuwania taji la Ligi kuu England, Manchester United inatarajiwa kuendeleza mbio zake za kuifukuza Manchester City katika miezi miwili ya mwisho ya msimu.
    United imepitia katika njia ngumu na kutoka salama ikishinda dhidi ya Arsenal, Liverpool na Tottenham—wakati pia ilitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kupata sare ya 3-3 na Chelsea — hivyo kubaki inazidiwa pointi mbili na City zikiwa zimebaki mechi 11 ligi kuisha.
    Ikiwa inakabiliwa na mechi ya wapinzani wa jadi dhidi ya City Aprili 30, mechi zilizobaki za United ni rahisi mno kulinganisha na za wapinzani wao.
    Wanaanza na West Bromwich Albion, ambayo imeshinda mechi zake tatu zilizopita, lakini ni kibonde mno anayekwenda Old Trafford.
    Zikitoka kutolewa nishai katika mechi ya kwanza ya Europa League hatua ya 16 bora Alhamisi, Manchester zote lazima ziwahahakishie mashabiki wake kwamba hazina ‘hangover’ wakati zinaporejea kwenye Ligi Kuu mwishoni mwa wiki.
    Wakati United iliyolipigwa 3-2 nyumbani na Athletic Bilbao wanaikaribisha WBA leo, City waliopigwa 1-0 na Sporting Lisbon ugenini wataifuata Swansea, ambayo imefungwa mechi mbili tu kati ya mechi zake 13 za nyumbani msimu huu tangu ipande.
    City imeshinda mechi zake zake nne zilizopita za ligi, lakini itamkosa beki wake wa nguvu, Vincent Kompany aliyeumia Ureno.
    United iliifunga Tottenham 3-1 wiki iliyopita na kuwaacha kwa pointi 11 Suprs wanaofundishwa na Harry Redknapp katika nafasi ya tatu.
    Baada ya kupigwa mechi mbili mfululizo na Arsenal na United, Spurs leo wanatarahjiwa kujipoza machungu kwa Everton, wakiwa wanaizidi kwa pointi nne Arsenal inayoshika nafasi ya nne.
    Arsenal iliyotolewa ‘kiume’ katika Ligi ya Mabingwa, itaikaribisha Newcastle Jumatatu, wakati Chelsea inayoshika nafasi ya tano itakuwa mwenyeji wa Stoke hiyo ikiwa mechi ya kwanza ya ligi ya Roberto Di Matteo tangu arithi mikoba ya boasi wake, Villas-Boas.
    Liverpool wanaweza kuwa nao tena Steven Gerrard na Glen Johnson waliokuwa majeruhi katika mchezo wa leo na Sunderland.
    Wigan itaifuata Norwich kesho, wakati Bolton itakuwa mwenyeji wa Queens Park Rangers na Wolverhampton Wanderers watakuwa nyumbani wakiikaribisha Blackburn leo. Fulham watasafiri kuwafuata Aston Villa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HASIRA ZA MAN UTD, MAN CITY LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top