// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GERRARD APIGA MATATU MECHI YA 400, LIVERPOOL YAUA 3-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GERRARD APIGA MATATU MECHI YA 400, LIVERPOOL YAUA 3-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2012

    GERRARD APIGA MATATU MECHI YA 400, LIVERPOOL YAUA 3-0


    Steven Gerrard (kushoto) akishangilia bao lake la pili.
    KIUNGO Steven Gerrard jana amecheza mechi yake ya 400 ya Ligi Kuu ya England na kupiga mabao matatu peke yake akiiongoza Liverpool kushinda 3-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Everton.
    Gerrard alifunga bao la kwanza dakika ya 34 baada ya kufumua shuti lililowapita mabeki watatu na kipa Tim Howard. Kiungo huyo mkongwe wa England, baadaye alifunga mabao mawili kwa jitihada za Luis Suarez dakika ya 51 na dakika za majeruhi.
    Pamoja na ushindi huo, kuwa ndani ya Top-Four bado inaonekana kuwa maji marefu kwa Liverpool, ingawa sasa Wekundu hao wanaizidi pointi tano Everton wakielekea kwenye fainali ya Kombe la FA Jumapili dhidi ya Stoke.
    Tayari Liverpool imetwaa Kombe la Ligi na kujihakikishia kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao. Sasa inapigania kumaliza juu ya Everton kwa msimu wa saba mfululizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GERRARD APIGA MATATU MECHI YA 400, LIVERPOOL YAUA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top