MKONGWE Ronaldinho ni mmoja kati wachezaji wenye majina makubwa
waliojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Brazil cha kocha Mano Menezes kwa
ajili ya maandalizi ya awali ya michuano ya Olimpiki mjini London.
Kocha wa The Selecao ameteua wachezaji 52 wa nguvu kupigania
nafasi 18 za kwenda London.
Ronaldinho ambaye anafanya vizuri katika klabu yak Flamengo ya
nyumbani kwao hivi sasa, yuko kwenye kundi la wachezaji wanaowania nafasi tatu
maalum kwa wachezaji waliozidi umri wa miaka 23 sambamba na beki wa AC Milan Thiago
Silva, beki wa Barcelona Dani Alves na kipa wa Inter, Julio Cesar.
Mshambuliaji wa Milan, Alexandre Pato, beki wa Real Madrid,
Marcelo na beki wa Manchester United, Rafael nao pia wamo kikosini, sambamba na
nyota wanaocheza nyumbani wa Kibrazil Neymar, Lucas na Leandro Damiao.
Kikosi kamili cha Brazil cha watu 52 hiki hapa:
Adriano (Barcelona), Alex Sandro (Porto), Alexandre Pato
(Milan), Allan (Vasco), Andre (Atlético Mineiro), Bernard (Atletico Mineiro),
Bruno Uvini ( Tottenham), Daniel Alves (Barcelona), Danilo (Porto), David Luiz
(Chelsea), Dede (Vasco), Diego Alves (Valencia), Douglas Costa (Shaktar Donetsk),
Dudu (Dynamo Kiev), Elias (Sporting), Elkeson (Botafogo), Fagner (Vasco),
Fernandinho (Shaktar Donetsk), Fernando (Gremio), Gabriel (Cruzeiro), Gabriel
Silva (Novara)
Galhardo (Flamengo), Paulo Henrique Ganso (Santos), Giuliano
(Dnipro), Henrique (Granada),
Hernanes (Lazio), Hulk (Porto), Jefferson (Botafogo), Jonas
(Valencia), Juan (Internazionale),
Julio Cesar (Internazionale), Leandro Damiao (Internacional),
Lucas (Sao Paulo), Lucas Mendes (Coritiba), Luisao (Benfica), Marcelo (Real
Madrid), Marquinhos (Corinthians), Neto (Fiorentina), Neymar (Santos), Oscar
(Internacional), Philippe Coutinho (Espanyol), Rafael (Manchester United),
Rafael Cabral (Santos), Renan Ribeiro (Atletico Mineiro), Romario
(Internacional), Romulo (Vasco), Ronaldinho Gaucho (Flamengo), Sandro
(Tottenham), Thiago Silva (Milan), Wellington Nem (Fluminense), Willian Jose
(Sao Paulo).
0 comments:
Post a Comment