KLABU ya Espanyol ilitoka nyuma na kuwafunga Racing
Santander waliokuwa pungufu ya mchezaji mmoja mabao 3-1 katika mechi ya Ligi
Kuu ya Hispanian jana hivyo kubaki kwenye nafasi ya kuwania kucheza Ligi ya
Mabingwa.
Christian Stuani aliifungia Santander bao la kuongoza dakika
ya 12, lakini Joan Verdu akaunganisha pasi ya Sergio Garcia kusawazisha dakika
ya 26.
Mshambuliaji anayecheza kwa mkopo kutoka Inter Milan, Philippe Coutinho aliifungia dakika saba baadaye Espanyol na Hector Moreno akakamilisha matokeo ya 3-1 kwa bao la kichwa akiunganisha mpira wa adhabu wa Coutinho dakika ya 80.
Marcos Gullon alionyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 51 na kuiacha Santander na wachezaji 10.

0 comments:
Post a Comment