Cristiano Ronaldo |
ENGLAND na Ujerumani zinaweza zisiwe na timu kwenye robo
fainali ya Ligi ya Mabingwa kama Chelsea na Bayern Munich hazitoweza
kubadilisha matokeo ya kufungwa kwenye michezo ya kwanza.
Tofauti na Italia ligi ya Serie A, inayoshutumiwa kwa vurugu
za uwanjani, kupungua kwa mashabiki na kushuka kwa thamani ya ligi hiyi,
wanaweza kumaliza leo kwa timu zao tatu kufuzu kwa nane bora.
Chelsea ilifungwa 3-1 kwenye mchezo wa kwanza hivyo
wataingia leo kuwakabili Napoli ambao imeshinda mechi zake tano zilizopita za
ligi na Ijumaa iliyopita ilichakaza Cagliari kwa mabao 6-3.
Bayern waliolala kwa bao 1-0 kutokak wa FC Basel, timu
isiyotarajiwa pamoja na APOEL Nicosia, watalazimika kumaliza rekodi ya
kutokufungwa wa timu hiyo ya Uswisi kama wanataka kusonga mbele.
Kushindwa kufanya hivyo itakuwa mwisho wa ndoto wa timu hiyo
ya Bavaria kucheza fainali itakayofanyika kwenye uwanja wao wa Allianz Arena.
Michezo mingine leo, ni ule wa Claudio Ranieri atakuwa
akiwaongoza Inter Milan, mabingwa wa 2010 kufuta bao1-0 walilofungwa na
Olympique Marseille ili kusonga mbele, huku Real Madrid wakitakiwa kumaliza
kazi yao kwa CSKA Moscow baada ya kutoka sare 1-1 kwenye baridi kali ya Russia.
Washindi wa mechi hizo wataungana na mabingwa watetezi
Barcelona, mabingwa mara saba AC Milan, Benfica mabingwa mara mbili na timu
ndogo ya APOEL kwenye upangwaji wa ratiba ya robo fainali hapo Ijumaa.
Kuondolewa kwa Chelsea kuitaifanya Ligi Kuu ya England kwa
mara ya kwanza kukosa timu kwenye robo fainali tangu msimu wa 1995/96.
Arsenal ilitolewa wiki iliyopita, pamoja na kushinda3-0
dhidi ya Milan haukutosha kuwavusha baada kufungwa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza,
huku Manchester United na Manchester City zikishindwa kufuzu hatua ya makundi.
Mabingwa wa Ujerumani, Borussia Dortmund walitolewa hatua ya
makundi huku Bayer Leverkusen wakizamishwa na Barcelona, kwa kufungwa 7-1
kwenye Uwanja wa Nou Camp wiki iliyopita kwa ujumla wa mabao 10-2.
Hivyo kuicha Bayern Munich pekee kupeperusha bendera ya
Bundesliga, ambayo msimu ujao watapata nafasi ya kuingiza timu tatu moja kwa
moja kwa hatua ya makundi kutokana na udhaifu wa Serie A.
Napoli, ikiwa kwenye msimu wake mzuri na kukumbusha enzi za
Diego Maradona walipotamba kwenye michuano ya Kombe la Ulaya, lakini baada ya
hapo hajawahi kwenda mbele zaidi ya hatua ya pili.
ìEnzi za Maradona zimebaki kuwa za mafanikio zaidi katika
historia ya Napoli, lakini tunajihisi kuwa tunakaribia mafanikio hayo ni jambo
linalofanya tujisikie faraja,îalisema kocha wa Napoli, Walter Mazzarri.
Safu yake ya washambuliaji watatu Edinson Cavani, ambaye
amefunga mabao matano, Ezequiel Lavezzi na Marek Hamsik wametegeneza moja ya
safu hatari zaidi kwa sasa.
Chelsea wamebadilisha kocha tangu walipocheza mchezo wa
kwanza kwa kumteua Roberto Di Matteo kuchukua nafasi ya Andre Villas-Boas
aliyetimuliwa.
Basel itakuwa ikijaribu kuwa timu ya kwanza ya Uswisi kufuzu
kwa hatua ya nane bora tangu Grasshoppers ilipofanya hivyo msimu wa 1978/79
wakati huo wa Kombe la Ulaya.
Bayern imeshinda mechi 11 kati ya 12 za Ulaya ilizocheza
nyumbani, japokuwa waliondolewa kwenye hatua hiyo baada ya kufungwa 3-2 na Inter Milan kwenye Uwanja wao wa
Allianz Arena.
Ranieri alinusurika kidogo kukumbwa na janga la Villas-Boas
tangu alipofungwa 1-0 na Olympique na kushinda mchezo huo kumebaki taji pekee
kwa Inter ambayo kwa sasa imeporomoka hadi nafasi ya saba katika Serie A.
Kikosi cha Inter katika mchezo wa kwanza kilikuwa na
wachezaji wenye wastani wa miaka 31 na siku 331, wakivunja rekodi yao wenyewe
ya Ligi ya Mabingwa walipocheza na wachezaji wa umri wa miaka 31 na siku 317
mapema msimu huu walipoikabili Lille.
Real wakiwa kwenye kiwango cha juu wataikaribisha CSKA
jijini Madrid, kwenye mazingira yao ya kujidai tofauti na ile hali hewa ya
baridi ya Moscow.
Timu ya Jose Mourinho ilimaliza hatua ya makundi kwa
asilimia 100, japokuwa wanatakiwa kuwa makini na mshambuliaji wa CSKA nyota wa
Ivory Coast, Seydou Doumbia ambaye amefunga mabao matano katika mechi sita za
Ligi ya Mabingwa msimu huu na rekodi ya kufunga mabao 12 kati ya mechi 13
alizocheza za ligi hiyo kwa miaka miwili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment