// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DROGBA AUZA NGUO ZAKE, VIATU KUCHANGISHA FEDHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DROGBA AUZA NGUO ZAKE, VIATU KUCHANGISHA FEDHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 10, 2012

    DROGBA AUZA NGUO ZAKE, VIATU KUCHANGISHA FEDHA


    Drogba akiwa katika uzi wa Ivory Coast. 

    MFUKO wa Didier Drogba, leo utafanya hafla ya uchangishaji fedha katika hoteli ya Dorchester Hotel mjini London, lengo likiwa ni kukusanya kiasi cha pauni Milioni 3 kwa ajili ya mradui wa ujenzi wa hospitali nchini kwao Ivory Coast.
    Zoezi hilo la tatu kufanyika katikia mradi huo, linatarajiwa kuhusisha watru kibao maarufu, wakiwemo wanasoka nyota duniani na wanasiasa, alisema mshambuliaji wa Chelsea.
    Mazagazaga kibao, zikiwemo jezi za mchezaji huyo, rafiki zake na wachezaji wenzake, viatu, soksi na kadhalika vitauzwa kwenye zoezi hilo la hisani.
    “Sapoti ambayo foundation yangu imepata hadi sasa ni babu kubwa, lakini bado tuna kazi zaidi ya kufanya,” alisema Nahodha huyo wa Ivory Coast.
    Kituo cha afya cha Gigantic kinajengwa katika wilaya ya Attecoube mjini Abidjan, eneo la watu fukara ambalo linakosa hadi zana za kisasa za tiba.
    Drogba alisema tiba na huduma kwa ujumla katika hospitali hilo, zitakuwa zikitolewa bure.
    Mfuko huo (Didier Drogba Foundation) ulianzishwa mwaka 2007, kwa lengo la kushughulika na masuala ya kiafya na elimu Afrika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DROGBA AUZA NGUO ZAKE, VIATU KUCHANGISHA FEDHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top