Drogba |
Fedha
hizo zinafanya jumla ya Pauni Milioni 3 zilizochangishwa na mfuko wake kwa
ajili ya ujenzi wa hospitali nchini mwao, Ivory Coast.
Tukio
hilo lilivutia watu kibao maarufu kuanzia wanasoka nyota duniani, waburidishaji,
wanasiasa na nyota wa Chelsea, John Terry, Frank Lampard, Ashley Cole, Michael
Essien, Petr Cech, Branislav Ivanovic, Florent Malouda, Salomon Kalou, Paulo
Ferreira, Ross Turnbull na Hilario waliohudhuria kumsapoti mchezaji mwenzao.
Wachezaji
wa Arsenal, Bakary Sagna na Gervinho sambamba na Emmanuel Adebayor wa Tottenham
nao walihudhuria.
Kiasi
kizuri cha mchango kilitoka kwa watu binafsi, wakati kiasi cha pauni 240,000 kilitokana
na mauzo ya jezi, viatu, soksi, headbands na bidhaa nyingine.
Rapa
Muingereza, Wretch 32 alijishindia saa ya dhahabu baada ya kutoa mchango mkubwa.
Drogba
aliwashukuru wageni wake kwa kusema: “Sapoti ambayo mmeonyesha kwa foundation yangu
hadi sasa ni kubwa sana. Nina furaha uko hapa na umechangia kufanikisha ujenzi
wa hospitali hii.”
Kituo
cha afya chja Gigantic kitajengwa wilaya ya Attecoube mjini Abidjan, eneo la
watu masikini linalokosa vifaa vya kisasa vya huduma za afya.
Drogba
alisema ushauri na matibabu vitakuwa vikitolewa bure kwa watu masikini. Mfumo
wa Didier Drogba ulianzishwa mwaka 2007, kwa lengo la kusaidia matatizo ya afya
na elimu Afrika.
0 comments:
Post a Comment