DK Jiri Dvorak |
Hatua hiyo inafuatia kiungo mwenye asili ya DRC, Fabrice Muamba kuanguka uwanjani na kuzimia na hadi sasa amelazwa, ingawa ameanza kupata nafuu.
Ofisa Mkuu wa Tiba wa FIFA, Jiri Dvorak, amesema leo kwamba mpango huo utafanyika katika mkutano wa tiba Mei 23 na 24 mjini Budapest, Hungary.
"Tumekaribisha madokta wote wa timu za taifan kuangalia kwa kina matatizo ya moyo," alisema Dvorak.
Muamba anaendelea vizuri na hali yake sasa inaridhisha, dokta amesema leo.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 bado yupo kwenye cha wagongwa wenye uangalizi maalum katika hospitali ya London Chest alikolazwa tangu aanguke na kupoteza fahamu kwenye ya Robo Fainali Kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspur Machi 17, mwaka huu.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na hospitali hiyo na Bolton ilisema: "Fabrice Muamba bado yupo chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalum katika hospitali ya London Chest, ambako hali yake ni mbaya, lakini yuko vizuri.
"Anaendelea kuimarika katika kupata unafuu. Mwishoni mwa wiki alikuwa tayari anaweza kukaa mbali na kitanda kwa muda mfupi, kuangalia Televisheni na ameanza kula.
0 comments:
Post a Comment