DIRECTOR wa filamu, Jason Russell, ambaye filamu yake
inayomshambulia kiongozi wa wapiganaji wa Uganda, Joseph Kony, ilizagaa kwenye
mtandao wa internet, inaelekea amepata ugonjwa wa akili.
Shirika lilofanya filamu hiyo, liitwalo "Invisible
Children", limesema kuwa Bwana Russell amelazwa hospitali kutokana na
machofu, kiwiliwili kuwa kikavu, na njaa.
Shirika la "Invisible Children", lilisema zogo
lilozuka baada ya filamu hiyo, limesumbua roho za wanachama wote; na hasa Bwana
Russell.
Ripoti zinasema kuwa Jason Russell amekutikana hakujistri
sawasawa, akipiga kelele mabara-barani, mjini San Diego, California.
Filamu hiyo ya nusu saa, iliyotoa wito kuwa Joseph Kony
akamatwe, ilizagaa kwenye mitandao, na kuwasikitisha wengi, lakini baadhi ya
watu wanaona filamu haikueleza vita vya Uganda vilivyo.
0 comments:
Post a Comment