Watoto wa kiume wanawekeana mkwara, Haye kulia na Chisora kushoto
Haye anapambana ma msitu wa watu kumfuata Chisora
Chisora anamchimba mkwara Haye sambamba na kumsukumia konde
Haye anajibu konde kwa Chisora
MWEZI mmoja baada ya kugombana na David Haye katika mkutano
na Waandishi wa habari, Dereck Chisora leo amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa
kumpokonya leseni yake ya ndondi ya Uingereza.Mbabe huyo wa uzito wa juu mwenye umri wa miaka 28,
alipokonywa leseni yake kufuatia kikao cha saa nne cha bodi ya Ngumi Uingereza (BBBC)
kilichofanyika Machi 14, mwaka huu.“Kilichomo ndani ya rufaa yetu ni kwamba hatujaridhishwa na
suala zima,” alisema Frank Warren, peomota wa Chisora. “Dereck Chisora atasimama
upande wake kisha tutaona nini kitatokea.”Baada ya kupigwa na Vitali Klitschko mjini Munich, Februari
19, Chisora aliingia kwenye ugomvi na bingwa wa zamani wa WBA, Haye katika
Mkutano na Waandishi wa Habari. Kabla ya pambano lake hilo, Chisora alimchapa kibao kaka wa
mpinzani wake, Wladimir Klitschko kwenye zoezi la upimaji uzito na badaaye akiwa
ulingoni, akamwagia maji nje ya ulingo usoni wakati anamuangalia ndugu yake.Chisora alikuwa anatafutwa na Polisi wa Ujerumani baada ya
kupigana na Haye.BBBC iliamua kwamba Chisora “hastahili kumiliki leseni ya.” Lakini
Warren anakana uamuzi huo.Kama Chisora atarejeshewa leseni yake, Warren alisema anatarajia
watapanda ulingoni tena na Haye.“Naona pambano litakuja. Ni eneo mwafaka kwao kumaliza
tofauti zao,” alisema Warren.Pamoja na hayo, Haye bado anasakwa na Polisi wa Ujerumani na
pia atatakiwa kujibu tuhuma kadhaa iwapo ataamua kurejea ulingoni baada ya kutangaza
kustaafu.
Samuel Eto’o eyes CAF Exco seat
-
Cameroonian Football Football (FECAFOOT) president Samuel Eto’o is keen to
become a member of the Confederation of African Football (CAF)’s executive
com...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment