Capello |
ALIYEKUWA kocha wa England, Fabio Capello amepewa bonge la
ofa la kazi lenye maslahi mazuri kuifundisha timu ya taifa ya China, bongostaz
imeipata hiyo.
Amepewa ofa ya mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya dola
za Kimarekani Milioni 8 kwa mwaka kufundisha timu ya wakubwa na mtandao wa soka
ya vijana China.
bongostaz imezinasa za ndani zaidi kwamba Capello amekubali
kufanya kazi, ila tu kama Msaidizi wake atakuwa Franco Baldini, Menejua Mkuu wa
Roma, ambaye alikuwa naye Real Madrid na England.
Hata hivyo, Baldini amemuambia kocha huyo mwenye umri wa
miaka 65 kwamba atabakia Roma, aliyojiunga nayo Oktoba mwaka jana, hadi mwishoni
mwa msimu ndipo ataamua.
Chama cha Soka China kimeonyesha kipo tayari kumsubiri Capello
hadi mwishoni mwa msimu.
Kocha mwingine mwenye mafanikio Italia, aliyeipa Italia Kombe
la Dunia mwaka 2006, Marcello Lippi pia amekuwa akitajwa kutakiwa na China.
Inafahamika kwamba Lippi, ambaye pia hyena timu kwa sasa, anataka
kusubiri kuona ataopata wapi kazi katika timu za taifa za Ulaya baada ya Euro
2012, kabla ya kujitia kitanzi na FA ya China.
0 comments:
Post a Comment