// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA YANG'ANG'ANIWA NYUMBANI, SASA TOP FOUR HATIHATI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA YANG'ANG'ANIWA NYUMBANI, SASA TOP FOUR HATIHATI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 24, 2012

    CHELSEA YANG'ANG'ANIWA NYUMBANI, SASA TOP FOUR HATIHATI

    Frank Lampard wa Chelsea, kushoto, akichuana na Sandro wa Spurs .
    KLABU ya Chelsea ilipoteza nafasi nzuri ya kuikaribia Tottenham katika mbio za kuwania Nne Bora ya Ligi Kuu England jioni hii baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
    Sare hiyo inawaacha Chelsea nafasi ya tano, wakiwa nyuma kwa pointi tano kuifikia nafasi hiyo ambayo hutoa fursa ya kucheza Ligi ya Mabingwa, na Tottenham wanaoshika nafasi ya nne hawakuwa na bahati kwa kushindwa kuondoka na pointi tatu baada ya mara m bili kukaribia kufunga.
    Spurs waliokuwa wakipigania ushindi wa kwanza dhidi ya Chelsea katika ligi tangu 1990, walipata nafasi nyingi za kufunga mabao, lakini wakashindwa kutumia.
    Nafasi nzuri zaidi ni kipindi cha kwanza katika dakika mbili za majeruhi, wakati mshambuliaji wa Tottenham, Rafael van der Vaart alipopoteza nafasi nzuri ya kufunga kwa bao lililookolewa na Petr Cech na kuzuiliwa kwenye mstari wa lango na Ashley Cole.
    Nafasi pekee nzuri kwa Chelsea ilikuwa dakika ya 73 wakati mpira wa adhabu wa Juan Mata ulipogonga mwamba na kipa Tottenham, Brad Friedel akiwa amekwishapotea.
    Mechi nyingine ya leo ni kati ya Manchester City na Stoke, wakati Manchester United watacheza na Fulham Jumatatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YANG'ANG'ANIWA NYUMBANI, SASA TOP FOUR HATIHATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top