// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA, REAL MADRID ZAUA KWA STAILI MOJA, ZATINGA NANE BORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA, REAL MADRID ZAUA KWA STAILI MOJA, ZATINGA NANE BORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 15, 2012

    CHELSEA, REAL MADRID ZAUA KWA STAILI MOJA, ZATINGA NANE BORA

    Didier Drogba (katikati) akifunga kwa kichwa bao lililofungua neema.
    Kaimu Kocha wa Chelsea, Roberto Di Matteo akimkumbatia Fernando Torres baada ya kushinda mechi ya jana.
    MABINGWA wa kihistoria Ulaya, Real Madrid wamempa raha kocha wao Jose Mourinho kwa kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa usiku wa jana.
    Baada ya kushindwa kufika Robo Fainali kwa misimu sita mfululizo kabla ya kutua kwa Mourinho, mabingwa hao mara tisa wa michuano hiyo, wamefuzu kwa mara ya pili chini ya kocha huyo.
    Madrid ilijibu sare ya 1-1 iliyolazimishwa ugeninina CSKA Moscow ya Urusi kwa kushinda 4-1 jana kwenye mchezo wa marudiano, siku ambayo Cristiano Ronaldo alitupia nyavuni mab ao mawili na kutimiza mabao 42 msimu huu.
    Timu ya zamani ya Mourinho, Chelsea imeungana na Madrid katika droo ya Robo Fainali itakayopangwa kesho baada ya wao pia kushinda 4-1 na kulipa kisasi cha kufungwa 3-1 na Napoli ya Italia katika mchezo wa kwanza.
    Kipigo cha Italia kilichangi kocha Andre Villas-Boas kufukuzwa, lakini kocha aliyerithi  mikoba yake, Roberto Di Matteo aliyekuwa Msaidizi wake, jana ameshinda mechi ya tatu mfululizo tangu aishike timu.
    Bao la mkwaju wa penalti la Frank Lampard dakika ya 75, liliufanya mchezo uhamie kwenye muda wa nyongeza (deakika 120), ambako Branislav  Ivanovic akapiga bao la ushindi na kufanya Chelsea ishinde kwa matokeo ya jumla ya 5-4.
    Droo la kesho la Robo Fainali litahusisha timu kutoka nchi saba, ambazo ni mabingwa watetezi Barcelona, AC Milan, Bayern Munich, Marseille, Benfica na APOEL timu ngebni katika hatua hii.
    “Baadhi ya timu kubwa kama Manchester United, Arsenal au Inter Milan hazipo,” alisema Mourinho, ambaye alitwaa ndoo hiyo akiwa na FC Porto mwaka 2004 na Inter Milan 2010.
    Katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, Gonzalo Higuain aliifungia Madrid bao la kwanza dakika ya 26 baada ya kupokea pasi ya Kaka.
    Shuti kali la mbali la Ronaldo lilidondoshewa nyavuni na kipa Sergei Chepchugov dakika ya 55.
    Karim Benzema naye alitumbukiza nyavuni dakika ya 70, kabla ya Zoran Tosic kuwafungia wageni dakika saba baadaye.
    Lakini Benzema akamsetia Ronaldo kufunga la nne dakika za lala salama.
    Akitoka kufunga bao lake la 100 katika Ligi Kuumwishoni mwa wiki, Didier Drogba aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 29, akiunganisha krosi ya Ramires. Terry naye akafunga akiunganisha kona ya Frank Lampard mwanzoni tu mwa kipindi cha pili.
    Na baada ya mpira wa kichwa uliopigwa na Ivanovic kumgonga mkononi Andrea Dossena, Lampard akaenda kufunga kwa penalty na kufanya sare ya jumla ya 4-4.
    Ivanovic akamaliza kazi kwa bao lake la muda waq nyongeza na kuifanhya England iwe na timu angalau katika Robo Fainali.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA, REAL MADRID ZAUA KWA STAILI MOJA, ZATINGA NANE BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top