// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA NI MASHAMBULIZI MWANZO MWISHO LEO KUUA TIMU LA MARADONA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA NI MASHAMBULIZI MWANZO MWISHO LEO KUUA TIMU LA MARADONA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2012

    CHELSEA NI MASHAMBULIZI MWANZO MWISHO LEO KUUA TIMU LA MARADONA


    Drogba, ataibeba Chelsea leo?
    KLABU ya Chelsea leo itashambulia kuanzia dakika ya mwanzo katika kujaribu kumlipia kisasi Andre Villas-Boas aliyepigwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Napoli, timu ya zamani ya Maradona.
    Klab hiyo ya London imemfukuza kocha kijana Mreno, tangu mwezi uliopita baada ya mechi ya kwanza na sasa Mtaliano Roberto Di Matteo, amabye huu utakuwa mtihani wake wa kwanza Ulaya unaweza kuwa mwisho iwapo wachezaji wake wasipombeba.
    Chelsea wanaweza kutinga Robo Fainali, wakipigana kama ilivyofanya klabu nyingine ya Ligi Kuu, Arsenal ambao walishindwa kidogo walipokuwa kwenye mtihani mzito wiki iliyopiota.
    Arsenal walifungwa 4-0 katika mechi ya kwanza na AC Milan, lakini katika marudiano wakashinda 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-3.
    Kwa Chelsea, kazi ni nyepesi zaidi ya hiyo ikiwa Napoli wanasaka ushindi wa sita mfululizo katika mashindano yote.
    “Kuanzain dakika ya kwanza tutajaribu kutengeneza nafasi za kufunga mabao. Tunatambua wana washambuliaji wazuri na tunatakiwa kuwa makini na wao, lakini tutashambulian kuanzia dakika ya kwanza,"alisema winga Juan Mata.
    Bao la Mata dhidi ya Napoli katika mchezo wa kwanza limepunguza kazi, kwani sasa ushindi wa 2-0 mjini London leo utaiwezesha England angalau kuingiza timu moja Robon Fainali katika nafasi yao pekee iliyobaki.
    “Katika soka hakuna kisichowezekana na Stamford Bridge tumekuwa tuna matokeo mazuri katika Ligi ya Mabingwa, hivyo nafikiri tunaweza kufanya hivyo,"alisema Mspanyola huyo.
    “Mashabiki wote watakuwa wakitushangilia sisi, ni fainali yetu, nja tunaweza kufanya hivyo."

    FAIDA MUHIMU…
    Kurejea kwa John Terry kwenye kikosi cha kwanza katika mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu ambayo walishinda 1-0 dhidi ya Stoke City kunaweza kuimarisha safu yao ya ulinzi katika mchezo wa leo wa marudiano.
    Pamoja na hayo, kwa matumaini yote, Chelsea wanatakiwa kushinda mfululizo bila kuruhusu nyavu zao kuguswa tangu Di Matteo aanze kazi, wakikutana na timu ambayo ipo kwenye kasi nzuri.
    Napoli wanaingia kwenye mechi ya leo wakitoka kushindaa 6-3 dhidi ya Cagliari katika Serie A mabao yote yakifungwa na wachezaji tofauti.
    Wakati hawajawahi kushinda England, waliwahi kutoa sare ya 1-1 na Manchester City katika hatua ya makundi msimu huu, ambayo inaweza kuwajengea kujiamini hata kama wanaihofia Chelsea baada ya kile kilichofanywa na Arsenal dhidi ya Milan.
    “Tuna nafasi nzuri, lakini tutacheza kama mechi iko 0-0,”alisema beki Paolo Cannavaro.
    Kocha wa Napoli, Walter Mazzarri atakaa kwenye benchi leo, baada ya kiusitishwa kwa adhabu yake kuwa nje mechi mbili.

    Vikosi vinavotarajiwa:
    CHELSEA:
    1-Petr Cech; 2-Branislav Ivanovic, 24-Gary Cahill, 26-John Terry, 3-Ashley Cole; 8-Frank Lampard, 7-Ramires; 23-Daniel Sturridge, 10-Juan Mata, 5-Michael Essien; 11-Didier Drogba

    NAPOLI:
    1-Morgan De Sanctis; 14-Hugo Campagnaro, 28-Paolo Cannavaro, 6-Salvatore Aronica; 11-Christian Maggio, 23-Walter Gargano, 88-Gokhan Inler, 18-Juan Zuniga; 17-Marek Hamsik, 7-Edinson Cavani, 22-Ezequiel Lavezzi

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA NI MASHAMBULIZI MWANZO MWISHO LEO KUUA TIMU LA MARADONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top