// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BRAZIL YAMCHANA ANGETILE WA FIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BRAZIL YAMCHANA ANGETILE WA FIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 04, 2012

    BRAZIL YAMCHANA ANGETILE WA FIFA

    WAZIRI wa Michezo wa Brazil ametangaza kuwa serikali yake haitaki kushirikiana na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, baada ya malalamiko yake, ambayo alisema hayakubaliki.
    Bwana Valcke alilalamika juu ya matayarisho ya Brazili ya Kombe la Dunia la mwaka 2014.
    Aldo Rebelo alisema hayo baada ya Bwana Valcke kusema kwamba Brazil inaonesha kushughulishwa zaidi na kushinda Kombe la Dunia, kushinda kuitayarisha nchi kwa mashindano hayo.
    Alisema ujenzi wa viwanja vya michezo, miundo mbinu ya usafiri na mahoteli kwa ajili ya washabiki, umezorota na kwamba Brazil inahitaji kupiga teke tako, izindukane.
    Bwana Rebelo alisema maneno hayo yanakera, na hayalingani na tathmini njema ya awali iliyotolewa na FIFA.
    Waziri huyo aliongeza kusema kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na FIFA - lakini siyo na Bwana Valcke.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRAZIL YAMCHANA ANGETILE WA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top