SHABIKI amepigwa risasi hadi kufa na watatu wamelazwa
hospitali wakiwa na hali mbaya baada ya mapambano ya mashabiki wa timu pinzani
nchini Brazil Jumapili.
Andre Alves, mwenye umri wa miaka 21, aliuawa kwa risasi ya
kichwani katika vurugu zilizohusisha mashabiki karibu 500 kabla ya mechi kati
wapinzani Corinthians na Palmeiras.Mmoja kati ya mashabiki watatu waliojeruhiwa vibaya, alipigwa risasi kwenye nyonga na anatakiwa kufanyiwa upasuaji.
Bado haijafahamika hali ya majeruhi wengine ikoje. Watu watatu walitibiwa na kuruhusiwa.
Mwaka jana, shabiki wa Corinthians aliuawa na mashabiki wa Palmeiras kabla ya timu hizo kumenyana kwenye Ligi ya Brazil, lakini hakuna mtu aliyekamatwa.
Corinthians ilishinda 2-1 jana kwenye Uwanja wa Pacaembu.
0 comments:
Post a Comment