// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BENZEMA ARUDI KAZINI REAL MADIRD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BENZEMA ARUDI KAZINI REAL MADIRD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 10, 2012

    BENZEMA ARUDI KAZINI REAL MADIRD


    Karim-Benzema mazoezini jana

    MSHAMBULIAJI Karim Benzema amerejea kazini Real Madrid na leo anatarajiwa kuwamo katika kikosi cha timu hiyo kinachoifuata Real Betis kwenye La Liga, baada ya wiki tatu za kuwa nje kwa sababu ya maunmivu.
    Mfaransa huyo hajacheza tangu atolewe nje baada ya kuumia katika sate ya 1-1 na CSKA Moscow kwenye Ligi ya Mabingwa mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora, Februari 21, lakini anaweza kucheza kwenye mechi ya marudiano Jumatano ijayo.
    “Natumaini atakuwa tayari kucheza kesho (leo) kama haitakuwa na athari yoyote,”alisema jana kocha Jose Mourinho katika mazoezi ya mwisho kabla ya mechi ya leo.
    "Kama kutakuwa kuna athari yoyote, hatutamchezesha wakati tuna miezi miwili zaidi katika michuano hii."
    Benzema ni mfungaji bora wa pili katika klabu hiyo baada ya Cristiano Ronaldo, akiwa ametikisa nyavu mara 21 katika mashindano yote.
    Angel Di Maria na Fabio Coentrao wapo nje kwa sababu ya majeruhi, wakati Ricardo Carvalho anatumuikia adhabu. Real inaongoza ligi kwa pointi zake 67 na ina mechi 13 zaidi kabla ya kumaliza ligi hiyo, ikiwazidi pointi 10 mabingwa watetezi, Barcelona wanaoshika nafasi ya pili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENZEMA ARUDI KAZINI REAL MADIRD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top