Nicklas Bendtner (kushoto) akishangilia bao lake na James McClean (kulia) |
MSHAMBULIAJI wa Denmark, Nicklas Bendtner alipiga bao pekee
la ushindi kipindi cha pili na kuiwezesha Sunderland kuifunga Liverpool 1-0 katika
mechi ya Ligi Kuu ya England jioni hii, kipigo ambacho kinawapunguzia Wekundu
wa Anfield nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Shuti la Fraizer Campbell liligonga mwamba, likamgonga kipa
wa Liverpool, Jose Reina kichwani na mpira ukamkuta Bendtner aliyeutumbukiza
nyavuni.
Liverpool iliyocheza ovyo ile mbaya, haikumsumbua kipa wa Sunderland,
Simon Mignolet na sasa inazidiwa pointi 10 katika vita ya kuwania nafasi ya nne,
iliyo wazi kwa Arsenal na Chelsea, ambao wanalingana kwa pointi.
Bendtner alitolewa nje baada ya jkuchanika dakika ya 83
alipogongana na beki wa Liverpool, Martin Skrtel.
0 comments:
Post a Comment