// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BAYERN YAFANYA MAUAJI, GOMEZ NI NOMA, INTER KWAHERI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BAYERN YAFANYA MAUAJI, GOMEZ NI NOMA, INTER KWAHERI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2012

    BAYERN YAFANYA MAUAJI, GOMEZ NI NOMA, INTER KWAHERI


    Kikosi cha Inter kilichoaga Ulaya
    WIKI moja baada ya Lionel Messi kuibuka mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano kwenye Ligi ya Mabingwa, mshambuliaji wa Ujerumani, Mario Gomez alikaribia kufuikia rekodi hiyo jana alipoiongoza Bayern Munich kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
    Gomez alikuwa mchezaji wa nane kufunga mabao manne kwenye moja wakati mabingwa hao mara nne Ulaya wakiiadhibu FC Basel mabao 7-0 na kulipa kisasi cha kupigwa 1-0 katika mchezo wa kwanza hivyo kufuzu kwa matokeo ya jumla ya 7-1.
    Arjen Robben pia alipiga mabao mawili kwa Bayern, ambayo inaungana na Marseille kufuzu kwa hatua inayofuata licha ya kiufungwa na Inter Milan 2-1.
    Mshabuliaji wa Inter, Diego Milito alisawazisha na jkufanya sare ya jumla ya 1-1 hivyo mchezo kuhamia kwenye dakika za nyongeza kabla ya kila timu kufunga na kufanya sare ya 2-2, hivyo wageni kunufaika kwa faida ya bao la ugenini.
    Marseille inaingia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1993.
    Kipa Steve Mandanda wa Marseille aliyeokoa mabao mengi ya wazi alitolewa nje kwa kadi nyekundu akisababisha na penalti ambayo ilitupiwa kwenye kamba na Giampaolo Pazzini, ingawa haikuisaidia Inter kusonga mbele.
    Mandanda atakosa mechi za Robo Fainali, hatua ambayo Marseille inaweza kukutana na Messi na mabingwa watetezi, Barcelona, mabingwa mara saba AC Milan, mabingwa mara mbili Benfica au ‘wa kuzuka’ APOEL Nicosia.
    Mabingwa wa kihistroria wa michuano hiyo, (mara tisa) Real Madrid watatafuta nafasi ya kusonga mbele kwenye Uwanja wa nyumbani kwa kumenyana na CSKA
    Pamoja na kushinda kufikia rekodi ya Messi, lakini Gomez amefikia rekodi ya Dado Prso mwaka 2003, kufunga mabao manne ndani ya dakika 23.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAYERN YAFANYA MAUAJI, GOMEZ NI NOMA, INTER KWAHERI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top