Mashabiki wa Azam wakifurahia ushindi wa leo |
AZAM
imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kutimiza
pointi 41, kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga iliyokuwa na wahezaji tisa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Mabao
ya Azam ambayo hata hivyo imecheza mechi mbili zaidi dhidi ya Simba inayoshika
nafasi ya pili kwa pointi zake 40 na Yanga ya tatu yenye pointi 40 pia, yalitiwa
nyavuni na kinara wa mabao Ligi Kuu John Raphael Bocco ‘Adebayor’ dakika ya nne
na 82 na lingine Kipre Balou kutoka Ivory Coast dakika ya 55.
Bao
la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi
Kiiza dakika ya 32.
Katika
mechi hiyo iliyotawalia na ubabe baina ya wachezaji wa timu hiyo, Yanga ilipatra
hasara ya kupoteza wachezaji wawili, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 16
tu na kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima dakika ya 13.
Cannavaro
alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja na Niyonzima alipewa kadi ya pili za
njano.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Yanga kilikuwa; Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Stefano
Mwasyika, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nurdin Bakari, Omega
Seme, Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza na Shamte Ally.
Azam:
Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Said Mourad, Bolou
Kipre, Kipre Tchetche, Ibrahim Mwaipopo/Abdi Kassim 'Babbi' dk 46, John Bocco, Salum Abubakar/Abdulhalim Humud dk 84 na Mrisho
Ngassa.
0 comments:
Post a Comment