Cannavaro akimlinda kipa |
KLABU ya Azam FC inataka kumkatia rufaa beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga kuichezea
timu yake katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union,
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Azama wanalalamika kwamba Cannavaro alipewa kadi nyekundu kwenye
mechi kati yao na Yanga na alitakiwa kukosa mechi tatu na kwamba adhabu yake
haihusiani na wachezaji waliositishiwa adhabu na Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi
ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Alfred Tibaigana.
Kiongozi mmoja wa Azam, ameiambia bongostaz kwamba hata wakati
Tibaigana anatangaza kusitisha adhabu za wachezaji wa Yanga alisema wazi
haingilii adhabu zilizotolewa moja kwa moja uwanjani.
“Mfano sisi, mchezaji wetu Salum Abubakar alipewa kadi
nyekundu na akakosa mechi tatu, iweje Yanga wa kwao akose mechi mbili tu?”alilalamika
kiongozi huyo.
Ikumbukwe Azam inawania moja kati ya nafasi mbili za juu kwenye
msimamo wa Ligi Kuu ili iwakilishe nchi katika michuano ya Afrika na ushindi wa
jana wa Yanga ni kama unapunguza matumaini yao kupata nafasi hiyo.
Simba inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 50, baada ya kucheza
mechi 22, wakati Yanga ina pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 na Azam imeshuka
hadi nafasi ya tatu kwa pointi zake 44
0 comments:
Post a Comment