// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AVB AMEBAKI HISTORIA STAMFORD BRIDGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AVB AMEBAKI HISTORIA STAMFORD BRIDGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 05, 2012

    AVB AMEBAKI HISTORIA STAMFORD BRIDGE

    YAMETIMIA. Klabu ya Chelsea ya England imempiga chini kocha wake kinda, Andre Villas-Boas jana.

    Kocha huyo mwenye umri wa miaka 34 amepoteza kazi hiyo saa 24 baada ya kupoteza pambano la Ligi Kuu dhidi ya West Bromwich Albion 1-0 juzi.
    Kufuatia mechi ya juzi Chelsea ilijikuta katika nafasi ya tano kweenye msimamo wa Ligi.
    Taarifa ya Chelsea imesema kuwa, aliyekua Kocha Msaidizi wa Boas, Roberto Di Matteo atakaimu nafasi hiyo hadi mwisho wa msimu.
    Villas-Boas, alituwa Stamford Bridge akitoka FC Porto ya Ureno Juni mwaka jana na ametimuliwa kwa matokeo yasiyo ridhisha yaliyoiacha Chelsea katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi, hali ambayo inaiweka klabu hio ukingoni kukosa kushiriki Ligi ya mabingwa barani Ulaya mwakani. Pamoja na hayo Chelsea ilichapwa 3-1 dhidi ya Napoli.
    Kocha huyo inasemekana alijenga uhasama baina yake na wachezaji wakuu katika klabu ya Chelsea, akiwemo kiungo Frank Lampard na vilevile mfululizo wa matokeo mabovu akiweza tu ushindi mara moja katika mechi saba.
    Matokeo haya hasa ndio yaliyosababisha mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich kumchukulia hatua.
    Msumari wa mwisho ulitokea jumamosi baada ya Chelsea kupoteza mechi dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion 1-0 kupitia Garth McAuley.
    Taarifa ya bodi ya Chelsea iliyotangaza kuvunjika kwa ndoa kati ya Chelsea na Villas Boas, imesifu juhudi zake na kusikitika kua hawakuweza kudumu zaidi ya hapa kutokana na matokeo mabovu na kukosekana kwa dalili kua hali hio inaweza kubadilika.
    Villas Boas aliletwa Chelsea kubadili kikosi kichovu baada ya ushindi wake wa vikombe vinne akiwa na klabu ya Porto msimu uliopita, lakini mda wake na Chelsea uligubikwa na habari za mvutano kama ulioarifiwa na Ma meneja waliomtangulia kua ndio uliosababisha kushindwa kuiongoza Chelsea na hivyo kutimuliwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AVB AMEBAKI HISTORIA STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top