Theo Walcott akifunga |
MABAO ya Kieran Gibbs, Theo Walcott na Mikel Arteta yameipa Arsenal
ushindi wa 3-0 dhidi ya Aston Villa, hiyo ikiwa ni mechi ya saba mfululizo
Washika Bunduki wa London wanashinda.
Arsenal sasa ni ya tatu kwa kufikisha pointi 58, baada ya
kucheza mechi 30 na Tottenham iliyotoa sare ya 0-0 na Chelsea ya nne kwa pointi
zake 55 iliyovuna kwenye mechi 30 pia.Bolton Wanderers ilirejea kazini baada ya siku saba tangu Fabrice Muamba aanguke na kupoteza fahamu kwa matatizo ya moyo, kwa kuichapa Blackburn Rovers mabao 2-1 kwenye Uwanja wa The Reebok, mabao yote yakitiwa kimiani na Wheater dakika ya 28 na 35, wakati la Blackburn lilifungwa na Nzonzi dakika ya 56.
Kiungo Muamba anaendela kupata nafuu hospitali tangu tukio hilo kwenye ya Robo Fainali Kombe la FA dhidi ya Tottenham.
Wigan imeichapa mabao 2-1 Liverpool inayosuasua kwenye Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Anfield leo na kujivuta katika jitihada zake za kuepuka kushuka daraja.
Beki Gary Caldwell aliipigia bao la ushindi dakika ya 63 Wigan, ambayo inabakia kwenye eneo la hatari, lakini sasa inalingana kwa pointi na Queens Park Rangers inayoshika nafasi ya tatu kutoka mkiani.
Mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez alipiga bao lake la 12 msimu huu akiisawazishia Liverpool baada ya Wigan kupata bao la mapema lililofungwa na Shaun Maloney, lakini mwishowe Liverpool ikapoteza mechi ya pili mfululizo nyumbani katika Ligi Kuu.
Ikiwa imebakiza mechi nane, Liverpool inazidiwa pointi 13 na Tottenham inayoshika nafasi ya nne, ambayo hutoa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa, baada ya kuambulia ushindi katika mechi moja tu kwenye mechi, lakini bahati nzuri kwao wamekwishafuzu Europa League baada ya kutwaa Kombe la Ligi.
Katika mechi nyingine, Grant Holt aliifungia mabao mawili Norwich kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu, timu yake ikiwafunga Wolverhampton Wanderers mabao 2-1 leo na kuzidi kuwachimbia kaburi wapinzani wao hao katika Ligi Kuu ya Englan.
Holt ameifanya Wolves ipoteze mechi ya nne mfululizo kwa mabao yake ya dakika za 26 na 45, yanayomfanya atimize 12, kabla ya kupewa kadi ya pili ya njano dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho kwa kucheza rafu.
Winga Matt Jarvis aliifungia bao la kuongoza Wolves dakika ya 25, lakini bado wapo kwenye hatari ya kushuka daraja kufuatia ushindi wa Bolton wa 2-1 dhidi ya Blackburn leo.
Mabao ya Leighton Baines na Nikica Jelavic kipindi cha pili, yaliipa Everton ushindi wa 2-0 katika Ligi Kuu dhidi ya Swansea kwenye Uwanja wa Liberty leo.
0 comments:
Post a Comment