// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ARSENAL YAFA KIUME, VAN PERSIE AKOSA BAO LA WAZI LA KUSAWAZISHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ARSENAL YAFA KIUME, VAN PERSIE AKOSA BAO LA WAZI LA KUSAWAZISHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 07, 2012

    ARSENAL YAFA KIUME, VAN PERSIE AKOSA BAO LA WAZI LA KUSAWAZISHA

    Kiungo Mholanzi wa AC Milan, Mark Van Bommel (kulia) akiteta na Mholanzi mwenzake, anayechezea Arsenal, mshambuliaji Robin Van Persie baada ya mechi la jana.
    KLABU ya AC Milan imenusurika na kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa matokeo ya jumla ya ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Arsenal , kufuatia jana usiku kufungw3-0 na klabu hiyo ya London.
    Ushindi wa Milan 4-0 kwenye Uwanja wa San Siro unazima ndoto za Arsenal kusonga mbele licha ya kushindsa 3-0.
    Mabingwa wa Serie A waliduwazwa kipindi cha kwanza na mabao ya Laurent Koscielny, Tomas Rosicky na Robin van Persie aliyefunga kwa penalti.
    Milan, ambao wametwaa taji hilo mara saba, walizinduka kipindi cha pili na kuwabana wenyeji hadi kuvuna tiketi hiyo ya kuvuka hatua hiyo ya 16 bora, lakini mashabiki wake walikuwa wana hofu ya kufa katika hatua kama hii kwenye mechi ya marudiano na Deportivo Coruna mwaka 2004.
    Katika mchezo huo, Van Persie alipoteza nafasi ya wazi mno ya kufunga bao la kufanya matokeo yawe 4-4.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAFA KIUME, VAN PERSIE AKOSA BAO LA WAZI LA KUSAWAZISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top