// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ARSENAL NA NEWCASTLE LEO, LAZIMA UYAJUE HAYA KABLA YA GAME - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ARSENAL NA NEWCASTLE LEO, LAZIMA UYAJUE HAYA KABLA YA GAME - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 12, 2012

    ARSENAL NA NEWCASTLE LEO, LAZIMA UYAJUE HAYA KABLA YA GAME

    ARSENAL wanaikaribisha Newcastle United katika Ligi Kuu ya England leo usiku.
    The Gunners imekuwa ikizinduka na kushinda mechi zake tatu zilizopita ikitokea nyuma, zikiwemo dhidi ya Tottenham na Liverpool na katika Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita walikaribia kufuzu baada ya kuifunga  3-0 AC Milan, wakitoak kupigwa 4-0 katika mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora.
    Ndoto za Arsenal Ligi ya Mabingwa zimekufa kwa mara nyingine, lakini angalau wamerudi kwenye nafasi ya kucheza tena michuano hiyo ya Ulaya mwakani.
    Timu ya Arsene Wenger inaingia kupigania ushindi wa tano mfululizo katika Ligi Kuu, lakini watatakuwa kuwa makini mbele ya Newcastle, ambao wako vizuri msimu huu.
    Ikumbukwe msimu uliopita walikuwa wamekwishapigwa 4-0 na Gunners hadi mapumziko, lakini wakazinduka na kupata mabao manne ndani ya dakika 19 na kutengeneza sare babu kubwa na ya kihistoria katika Ligi Kuu ya England.


    KUHUSU TIMU:
    Mikel Arteta na Aaron Ramsey watarejea kwenye kikosi cha Arsenal baada ya kupona.
    Yossi Benayoun amepona na Andre Santos amerejea mazoezini baada ya matatizo ya muda mrefu ya kifundo cha mguu.
    Peter Lovenkrands wa Newcastle anawezaa kukosa mechi zote zilizobaki za msimu baada ya kuumia kwenye mechi na Sunderland.
    Lakini kocha Alan Pardew hana majeruhi zaidi wa kutisha kikosini mwake kuelekea mechi la leo.

    TAARIFA ZA MECHI:

    ARSENAL:
    •Arsenal wanasaka ushindi wa tano mfululizo katika Ligi Kuu.
    •Katika mechi zote tatu zilizopita, The Gunners wamekuwa wakitokea nyuma na kushinda. Kwa ujumla, wametokea nyuma na kushinda mechi tano za Ligi Kuu msimu huu. Hakuna klabu katika historia ya Ligi Kuu ambayo angalau imetoka nyuma na kushinda mechi nne.
    •Arsenal wamefunga mabao katika dakika za mwisho za mchezo katika mechi tatu kati ya mechi zao nne zilizopita.
    • Robin van Persie amefunga mabao 25 msimu huu, ikiwa ni pamoja na kufunga katika kila mechi kwenye mechi nne zilizopita nyumbani (mabao sita).

    NEWCASTLE
    • Newcastle wamefungwa mechi tatu kati ya mechi zao nne zilizopita kwenye Ligi Kuu.
    • The Magpies wameambulia pointi moja tu katika mechi tisa walizokwenda London msimu huu, wakifungwa na Tottenham na Fulham na kutoa sare na QPR.
    • Timu ya Alan Pardew imefungwa mabao matano matano katika mechi mbili kati ya tatu zilizopita za ugenini, wakipigwa 5-2 na Fulham na 5-0 na Tottenham.
    • Demba Ba amefunga mabao 16 Ligi Kuun msimu huu – ambayo ni mengi zaidi kwa mchezaji wa Newcastle katyika msimu mmoja tangu Alan Shearer afunge 22 msimu wa 2003/04.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL NA NEWCASTLE LEO, LAZIMA UYAJUE HAYA KABLA YA GAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top