// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); APR YATOLEWA AFRIKA, GOR MAHIA KIMENUKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE APR YATOLEWA AFRIKA, GOR MAHIA KIMENUKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 05, 2012

    APR YATOLEWA AFRIKA, GOR MAHIA KIMENUKA


    MABINGWA wa Ligi Kuu ya Kenya, Tusker wametolewa katika Ligi ya Mabingwa baada ya kufungwa 1-0 na APR mjini Kigali, Rwanda.
    Nyota wa Burundi, Papy Faty alipiga bao hilo pekee dakika ya 62 na kuzima ndoto za Tusker kusonga mbele.
    Mechi ya kwanza iliyochezwa Nairobi wiki mbili zilizopita iliisha kwa sare, kocha Mholanzi wa APR, Ernie Brandts amefurahia ushindi huo.
    Ilikuwa ni wiki ngumu kwa Wakenya, kwani hata Gor Mahia imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho na Ferroviario De Maputo kwa jumla ya mabao 3-0.
    Tusker ilitarajiwa kurejea Nairobi jana kuendelea na kampeni za kutetea KPL.
    Gor Mahia hivi sasa inataka kumfukuza kocha wake Mcameroon Anaba Awono kutokana na kiwango kibovu kinachoonyeshwa na timu hiyo na matokeo mabaya kwa ujumla.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: APR YATOLEWA AFRIKA, GOR MAHIA KIMENUKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top