Add captionBalotelli wa Man City |
WAPINZANI wa Jiji la Manchester, watarejea kwenye mawindo yao
ya taji la Ligi Kuu England baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ulaya, lakini
pia wakionekana kama kuporomoka kiwango.
Baada ya kutolwa kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa,
wametolewa pia na kwenye 16 Bora ya Europa League, hivyo wana sehemu moja tu
sasa ya kurudishia heshima, kwenye Ligi ya nyumbani, wanapofukuzana kuwania
taji.
Vinara wa England, Manchester United walishindwa kufikia
ubora wa timu inayoshika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania, La
Liga, Athletic Bilbao baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao 5-3, wakati City
waling’olewa na Sporting Lisbon ya Ureno.
"Tunatakiwa kutwaa ubngwa wa Ligi Kuu kuunusuru msimu
wetu. Kama hatutatwaa ubingwa wa Ligi Kuu, utakuwa msimu mbaya haswa,"alisema
beki wa United, Patrice Evra kuiambia MUTV.
"Sina wasiwasi na Ligi Kuu, kwa sababu wanacheza vizuri
na sasa tuko juu, mbele ya Manchester City."
United inawazidi pointi moja jirani zao hao wakiwa na pointi 67
walizovuna kwenye mechi 28 na wanaweza kufikisha pointi nne za kuwazidi
wapinzani wao hao Jumapili wakiifunga Wolverhampton Wanderers siku ambayo City hawatakuwa
na mechi hadi Jumatano watakapoikaribisha Chelsea.
Kama wataendelea kukamatana hivyo hivyo, basi bingwa
ataamuliwa kwenye mechi ya wapinzani wa Manchester, mwezi ujao kwenye Uwanja wa
Eastlands.
England imekuwa na mwaka mbaya msimu huu Ulaya, ikiingiza
timu moja tu katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa, Chelsea, hali inayokuja
miaka mitatu baada ya nchi hiyo kuingiza timu tatu kati ya nne kwenye Nusu
Fainali.
City angalau wanaweza kujifariji pamoja na matokeo mabaya
Ulaya zaidi ya United- kwanza walipangwa kundi gumu katika Ligi ya Mabingwa na
kutolewa Europa League na Sporting hakukuwa
kinyela kama kwa jirani zao.
Kocha Roberto Mancini anaamini wachezaji wake watapigana na
kutwaa taji la kwanza la Ligi Kuu tangu mwaka 1968.
0 comments:
Post a Comment