// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ANELKA AZUA KIZAAZAA CHINA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ANELKA AZUA KIZAAZAA CHINA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 09, 2012

    ANELKA AZUA KIZAAZAA CHINA

    Anelka katika jezi la Kichina
    WAKATI Ligi Kuu ya China inaanza Jumamosi ya kesho, Nicolas Anelka amekuw3a gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari, kwamba pamoja na matumaini ya kuvutia watu wengi uwanjani, lakini kitendo cha kumsajili mchezaji kama huyo ni mchezo mchafu. Kwa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Anelka klabu ya Shanghai Shenhua imejijengea umaarufu mkubwa na inatarajiwa kuvuna mashabiki wengi kwenye mechi zake kuanzia sasa, ingawa inatarajiwa kuwa na madhara sawa na aliyosababisha David Beckham Marekani.
    Na kwa matarajio ya kumnasa pia na ‘patna’ wake aliyekuwa naye Chelsea, Didier Drogba, klabu hiyo imeihifadhi jezi namba 11 ambayo itakizidi kuipatia umaarufu soka ya China kwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa.
    Klabu nyingine zinalaani vikali matumizi ya fedha kibao katika manunuzi ya wachezaji, yanayowahusisha pia mabingwa mara mbili mfululizo wa China, Guangzhou Evergrande.
    Kampuni ya Evergrande Real Estate iliwekeza fedha kibao Guangzhou FC mswishoni mwa mwaka 2009, ikinunua wachezaji kibao wa timu ya taifa ya China.
    Mwajka jana walisajili Wabrazil wawili akiwemo mchezaji bora wa mwaka wan chi hiyo, Dario Conca kwa kiasi cha Euro Milioni 10 kutoka klabu ya Fluminese ya Brazil.
    Muargentina huyo anacheza sambamba na washambuliaji wa Kibrazil, Cleo na Muriqui katika kikosi cha kutkosha ambacho kilimaliza juu ya Beijing Guoan walioshika nafasi ya pili 2011.
    Timu hiyo ya Kusini mwa China ilitoa onyo kali wiki hii, kwa kuwafunga Jeonbuk Hyundai Motors wa Korea Kusini mabao 5-1 ugenini katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa Asia. Timu hiyo iliyopigwa 5-1 mwaka jana ilifika fainali ya Mabingwa Asia.
    Anelka analipwa mshahara wa Euro 234 000 kwa wiki na Shanghai Shenhua imepandisha bei ya tiketi ya mechi zake kwa mara ya mbilizi ya bei ya awali, kutoka yuan 350 hadi 800.
    Mwanasoka wa zamani, Don O'Riordan, ambaye kwa sasa ni kocha Beijing, anasema nyota huyo wa nguvu wa Ufaransa atavutia kizazi kipya cha China kujitumbukiza kwenye soka.
    Wapinzani wao nao, Beijing Guoan pia wamepandisha bei ya tiketi zao kutoka yuan 360 hadi 500, baada ya kusajili wachezaji nyota.
    Idadi ya watazamaji katika viwanja China imepanda katika miaka ya karibuni kutoka wastani wa watu 10 500 mwaka 2006 hadi zaidi ya watu 17 500 mwaka jana. Pia, Chaneli ya Michezo China imefufua dili wa kutangaza (Ligi Kuu) CSL kwa msimu ujao.
    Hata hivyo, baadhi wanakandia kwamba fedha nyingi zimewekezwa katika CSL lakini fungu dogo tu ndio linakwenda kwenye mpango wa soka ya vijana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ANELKA AZUA KIZAAZAA CHINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top