Anelka |
MSHAMBULIAJI wa Kifaransa, Nicolas Anelka alipiga bao katika
mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Cbhina akiicheza timu yake mpya, Shanghai
Shenhua japokuwa ilifungwa mabao 3-2 na wapinzani wao wakubwa, Beijing Guoan.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Chelsea, aliisawazishia
timu yake mpya, Shenhua na kupata sare ya 2-2 katika mechi ya wapinzani wa jadi
wa China.
Timu ya Anelka ilikuwa imekwishaloa 2-0, shukrani kwao Piao
Cheng na kiungo Mreno, Manu.
Mshambuliaji wa Australia, Joel Griffiths alianza
kuisawazishia Shenhua, akiichezea mechi ya kwanza tangu ajiunge nayo kutoka Guoan
Januari, akifunga kwa penalti na kufanya 2-1.
Winga wa zamani wa Shanghai, Mao Jianqing alizima matumaini
ya timu yake ya zamani, akiifungia Beijing bao la ushindi dakika za lala salama,
katika mechi yake ya kwanza Guoan.
Jumamosi iliyopita, Anelka aliwaangusha mashabiki baadaya
kukosekana uwanjani katika mechi ya kwanza ya Shenhua katika Ligi Kuu ya China
dhidi ya Jiangsu Sainty, kutokana na kuwa majeruhi.
Mfaransa huyo alikuwa gumzo kuelekea mchezo huo kwenye Uwanja
wenye uwezo wa kumeza mashabiki 68 000, Uwanja wa Workers mjini Beijing, lakini
ilielezwea hakuwa fiti kiasi cha kutosha kucheza mechi hiyo.
Aliwasalimia mashabiki 150 waliokuwa Uwanja wa ugenini ambao
walijibu kwa furaha huku wakitaja jina la shujaa wao huyo mpya.
Baadhi ya mashabiki wa Shenhua wamesafiri kwa saa 15 kwenda kuishangilia timu yao.
"Nataka kusema, Nimekuja hapa kuisapoti timu na si
Anelka", alisema shabiki wa Shanghai, David Xie, "Lakini sina matumaini
na timu, hata kama amefunga bao lake la kwanza wakati timu yetu imepoteza
mchezo."
Anelka amekuwa mchezaji babu kubwa zaidi kuwahi kusajiliwa
katika historia ya ligi ya China baada ya kukubali kutua Shenhua, Desemba mwaka
jana kwa mshahara wa Euro 270 000 kwa wiki.
0 comments:
Post a Comment