MSHAMBULIAJI Allan Wanga alirejea kwa kishindo kwenye kikosi cha timu ya taifa, Harambee Stars akiiwezesha kushinda 2-1 dhidi ya Togo katika mechi ya kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 juzi.
Akirejea kikosini baada ya miaka miwili, Wanga aliwafungia wenyeji bao la ushindi dakiika ya 65 na kuitengenezea Kenya mazingira ya kufuzu. James Situma aliifungia Stars bao la kuongoza kabla ya The Hawks kusawazisha dakika tatu kabla ya mapumziko kupitia kwa Razak Boukari.
Dennis Oliech alikaribia kuifungia Kenya mabao dakika ya 49 na 58, lakini Nahodha huyo bahati yake haikuwa yake.
0 comments:
Post a Comment