Aguero |
WAGOMBEA taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester
City watamkosa mshambuliaji wao Sergio Aguero katika mchezo wa leo nyumbani
dhidi ya Sunderland baada ya kupata majeruhi ya kipumbavu mguuni, kocha Roberto
Mancini alisema jana.
"Ni majeruhi ya kipumbavu,"alisema Mancini katika
mkutano na waandishi wa habari. "Halikuwa kosa lake, lakini hawezi kucheza
na majeruhi haya; kwa siku moja, siku 10 au wiki mbili, sifahamu."
Mancini, ambaye tayari anaye Muargentina mwenzake Aguero, Carlos
Tevez hakuelezea kwa undani kuhusu majeruhi hayo.
"Nimesikitishwa mno, natumai, (si wiki kadhaa) kwa
sababu tumempoteza mshambuliaji wetu hodari kwa mambo ya kipumbavu. Hawezi kucheza
dhidi ya Stoke na hawezi kucheza kesho (leo). Natumai atakuwa tayari kwa ajili
ya Arsenal mwishoni mwa wiki ijayo."
City, ambayo inazidiwa pointi tatu na Manchester United, inaweza
kurejea kileleni ikiifunga Sunderland kwa sababu United hawachezi hadi Jumatatu
dhidi ya Blackburn Rovers ugenini.
Tevez amecheza mechi mbili akitokea benchi tangu arudishe
uhusiano mzuri na klabu yake baada ya kutofautiana kwa kugoma kuinuka kupasha
aingie kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich, Septemba mwaka
jana na Mancini amesema mchezaji huyo anaweza kuisaidia timu katika kampeni ya
ubingwa kwenye mechi nane zilizobaki.
"Anaimarika taratibu, lakini nafikiri anaweza kuanza,"alisema
Mancini. "Lakini nafikiri anaweza kucheza kwa muda zaidi, anaimarika kila
wiki."
City pia itampokea tena beki wake Vincent Kompany aliyekosa
mechi nne zilizopita kwa maumivu ya nyama.
Mbelgiji huyo ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba:
"Nimepata awamu ya pili ya mazoezi na timu. Kama mambo yatakwenda kama
yalivyopangwa nitakuwepo kwenye mechi na Sunderland."
Pia amewataka mashabiki wa City kuwa nyuma ya timu yao
kuisaidia itwae taji la kwanza tangu mwaka 1968.
"Ni mechi nane zilizobaki za msimu, natumai mashaiki
wapo tayari kupiga kelele kama ambavyo wamekuwa wakifanya siku zote na
tutahakikisha tunafanya mambo mazuri," alisema.
0 comments:
Post a Comment