Wachezaji wa AC Milan wakimpongeza Ibra |
AC Milan ilipiga hatua kubwa katika kulikimbilia taji la
Serie A kwa kutoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Roma kwenye Uwanja wa San
Siro usiku wa jana.
Pablo Osvaldo alifunga la kuongoza kipindi cha kwanza, lakini
The Rossoneri wakajibu kwa mabao mawili ya Zlatan Ibrahimovic kipindi cha pili
hivyo timu ya Massimiliano Allegri imebeba pointi tatu muhimu, kuelekea kwenye
Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona.Kwa ushindi huo, AC Milan imefikisha pointi 63 ikining’inia kileleni mwa msimamo wa Serie A, wakati Roma iko nafasi ya sita kwa pointi zake 45.
The Rossoneri watakuwa wenyeji wa Barcelona Jumatano, kabla ya wao pia kwenda Camp Nou wiki ijayo, wakati Giallorossi watakuwa wenyeji wa Novara.
0 comments:
Post a Comment