WAKIWA kwenye kiwango kizuri, Catania hakika wanaitia presha
vinara wa Serie A, AC Milan.
Kocha Vincenzo Montella atawakosa beki Alessandro Potenza na
kiungo Marco Biagianti kwa sababu ni majeruhi, lakini beki wa pembeni Marco
Motta yupo kikosini tena licha ya Pablo Barrientos kupewa nafasi kubwa ya kuanza
kama kiungo wa kulia.
Kiungo mchezeshaji, Fracesco Lodi, anaweza kuongoza timu
hiyo katika dimba la kati akiwatengenezea nafasi za kufunga Alejandro Gomez na
Gonzalo Bergessio.
Ikionekana kuwa na safu imara ya ulinzi baada ya kuikomalia
Barcelona kwa sare ya 0-0 katika Ligi ya Mabingwa, Milan ina makovu kadhaa.
Kiungo Sulley Muntari na beki wa kushoto Djamel Mesbah wanatumikia
adhabu. Mark van Bommel atakuwapo tena baada ya kumaliza adhabu, lakini kuwepo
kwa mkongwe Alessandro Nesta, anaweza kupumzishwa kwa ajili ya mechi ya
marudiano na Barca Jumanne.
Beki wa kati Thiago Silva anaendelea kuuguza maumivu yake
baada kwenye mechi ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Roma na kwa manaa hiyo, Gianluca
Zambrotta na Daniele Bonera kwa mara nyingine wataanza kwenye kikosi cha
kwanza, licha ya kupona kwa Ignazio Abate.
Wakati huo huo: mshambuliaji Maxi Lopez anaweza kucheza
dhidi ya timu hiyo aliyoikimbia majira ya baridi msimu huu kuhamia San Siro, lakini
inaonekana anaweza akaanzia benchi akiwapisha Zlatan Ibrahimovic na Stephan El
Shaarawy.
JE WAJUA?
Catania imefungwa mechi moja tu katika mechi zake 10 zilizopita,
3-1 dhidi ya Juventus Februari 18 mjini Turin.
The Sicilians wamefungwa mechi mbili tu Uwanja wa Angelo
Massimino msimu huu na sasa wanashika nafasi ya saba katika Serie A.
Catania ilifungwa 4-0 na The Rossoneri Novemba, mwaka jana Uwanja wa
San Siro.
AC Milan imeshinda mechi zake zote nne zilizopita Serie A, huku
Ibrahimovic akifunga mabao saba katika kipindi hicho.
Vijana wa Massimiliano Allegri, wameshinda mechi 10 ugenini
katika Serie A msimu huu, ikiwa ni mechi nyingi kuliko timu zote msimu huu.
Ni timu yenye wachezaji wengi waliofunga mabao, ikiwa
wachezaji wake 17 tofauti wameifungia mabao Milan msimu huu.
Vikosi;
CATANIA: Carrizo, Belluschi, Legrottaglie, Spolli, Barrientos,
Izco, Lodi, Almiron, Marchese, Bergessio na Gomez.
AC MILAN: Abbiati, Zambrotta, Bonera, Mexes, Antonini, Aquilani,
Ambrosini, Nocerino, Boateng
Ibrahimovic na El Shaarawy.
0 comments:
Post a Comment