BILIONEA Roman Abramovich anaweza kumuangukia Jose Mourinho,
baada ya kocha huyo wa zamani wa Chelsea, kupendekezwa kwa kiasi kikubwa kurejea
Stamford Bridge msimu ujao kupiga tena kazi, kufuatia kutimuliwa kwa Andre
Villas-Boas.
Abramovich amemwaga Villas-Boas Jumapili zikiwa ni saa 24 baada
ya kipigo cha 1-0 kutoka kwa West Bromwich Albion, kinachowaangushia The Blues nafasi
ya tano katika Ligi Kuu.
Kiungo wa zamani wa Chelsea, Roberto Di Matteo, ambaye
alikuwa akifanya kazi msaidizi wa Villas-Boas, amepewa ukocha wa muda hadi
mwsiho wa msimu.
Mtihani wa kwanza wa Di Matteo ni mechi ya marudiano ya
Raundi ya Tano Kombe la FA dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza, Birmingham kwenye
Uwanja wa St Andrews kesho.
Baada ya hapo, Mtaliano huyo atakuwa na kibarua cha
kuirudisha Chelsea kwenye Top Four, inayowahakikishia kucheza Ligi ya Mabingwa
msimu ujao na pia atakuwa na kibarua cha kuupiku ushindi wa 3-1 walioupata
Napoli katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa.
Lakini habari rasmi ni kwamba, Abramovich sasa anasaka kocha
wa nane katika miaka nane ya kuimiliki klabu hiyo ya Magharibi mwa London.
Tangu ainunue Chelsea mwaka 2003, Abramovich amewafukuza Claudio
Ranieri, Mourinho, Avram Grant, Luiz Felipe Scolari, Carlo Ancelotti na sasa Villas-Boas.
Kocha wa Real Madrid, Mourinho ameiwezesha timu hiyo
kuongoza Ligi Kuu ya Hispania, La Liga licha ya ushindani mkubwa kutoka kwa Barcelona.
Tayari Mourinho anahisi hapendwi Hispania, kutokana na
misukosuko na uhusiano mbaya uliojengeka
kati yake na wadau wa timu hiyo na vyombo vya habari.
Bado anawasiliana kwa sms na watu wazito ndani ya Chelsea nab
ado anapendwa sana Stamford Bridge na wachezaji na mashabiki.
Kudhihirisha tetesi hizo, Mourinho alionekana London wiki
iliyopita akinunua nyumba mpya.
Watu wa karibu na Mreno huyo wanasema yuko tayari kurejea
England na inaelezwa hivi sasa yupo kwenye mawasiliano mazuri na Abramovich baada
ya kuondoka Chelsea, Septemba mwaka 2007.
Kocha wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez, ambaye kwa
sasa hana kazi baada ya kutupiwa virago Inter Milan, naye anatajwa kuwa kocha
mpya wa Chelsea.
Wengine ni kocha wa Barcelona, Pep Guardiola, ambaye
amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa wa Hispania na labda yu tayari kwa
changamoto mpya baada ya mafanikio makubwa Nou Camp.
0 comments:
Post a Comment