// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ZAMBIA WAPOKEWA KWA SHANGWE ZA KUFA MTU LUSAKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ZAMBIA WAPOKEWA KWA SHANGWE ZA KUFA MTU LUSAKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 14, 2012

    ZAMBIA WAPOKEWA KWA SHANGWE ZA KUFA MTU LUSAKA

    Mabingwa wapya wa soka wa Afrika, Chipolopolo wa Zambia wamepokelewa kwa shangwe katika mji mkuu Lusaka.
    Mwandishi wa BBC anasema mashabiki waliokuwa wakisubiri, walilipuka kwa kelele za shangwe, wakati nahodha Christopher Katongo alipotoka kwenye ndege akiwa amelibeba Kombe la dhahabu la Mataifa ya Afrika.
    Zambia waliwashinda Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 8-7, katika mchezo wenye msisimko hasa baada ya dakika za kawaida na za nyongeza kumalizika."Hakutukata kuondoka mikono mitupu "Kennedy MweeneUshindi huu una umuhimu wa kipekee hasa kwa sababu miaka 19 iliyopita karibu kikosi kizima cha Zambia kiliteketea katika ajali ya ndege nchini Gabon. Mwandishi wa BBC Mutuna Chanda anasema barabara ya kwenda uwanja wa ndege wa Lusaka imetapakaa rangi ya ijani, nyekundu, machungwa na nyeusi, huku maelfu ya mashabiki wakijipanga kutaka kuwaona wachezaji wakirejea rasmi.Kutakuwa na sherehe katika viwanja vya wazi mjini Lusaka.KutuzaTakriban watu 1,000, wengi wao wakiwa wametembea kilomita 25, walikuwepo uwanjani kuwalaki wachezaji wa timu ya taifa.Shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na rais wa zamani Rupiah Banda na Kenneth Kaunda, ambao wote ni mashabiki wakubwa wa kandanda.Wananchi wengi wa Zambia wamejipa likizo hii leo ili kusherekea ushindi wa kwanza kabisa wa Zambia wa Kombe la Mataifa ya Afrika.Kikosi hiki kilichoibuka na ushindi, kiliondoka katika uwanja ule ule wa ndege wa Libreville, ambao ndege ya kijeshi iliongeza mafuta ikielekea Senegal kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi Machi 1993 - na ndege hiyo kuanguka muda mfupi baada ya kupaa.Wachezaji wa Zambia, maarufu kama Chipolopolo Boys (yaani risasi za shaba), walitoa heshima zao kwa wachezaji 18 waliokufa katika ajali hiyo ya ndege - na kutuza ushindi huu kwa kikosi hicho kilichopotea.Amani"Wachezaji waliokufa katika ajali ya ndege nchini Gabon ndio walitupa hamasa, na nguvu katika michuano hiyo," amesema golikipa Kennedy Mweene akiwaambia waandishi wa habari kabla ya kuondoka Libreville."Hatukutaka kuondoka mikono mitupu," alisema.Winga Felix Katongo aliwaambia waandishi wa habari: "Tulitaka kushinda kombe hili ili wananchi wa Zambia wajivunie na kwa wale waliokufa, kupumzika kwa amani. Sasa roho zao zitakuwa na amani."
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAMBIA WAPOKEWA KWA SHANGWE ZA KUFA MTU LUSAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top