NAAM, ilikuwa miezi, wiki, siku na hatimaye sasa zimebaki
saa chache tu kabla ya mpambano mkali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kati ya
mabingwa wa Tanzania Yanga dhidi ya Zamalek ya Misri kesho Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Zamalek tayari wapo Dar es Salaam na wamefikia Kempisnky Hotel, pembezoni mwa bahari ya Hindi wakati Yanga wamejichimbia mtaa kama wa tatu kutoka walipo wapinzani wao, JB Belmonte Hotel, barabara ya Azikiwe.
Yanga itakutana na mabingwa hao wa Afrika mara tano katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana wiki mbili baadaye mjini Cairo.
Yanga itashuka dimbani Jumamosi ikiwa katika hali nzuri kimchezo, ikitoka kushinda mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 3-1 mara mbili dhidi ya JKT Ruvu na Mtibwa Sugar na 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Kihistoria hii itakuwa ni mechi ya tatu kuzikutanisha Yanga na Zamalek, awali mwaka 2000 zilimenyana mara mbili katika iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi Afrika.
Yanga ilitolewa kwa jumla ya mabao 5-1, ikilazimishwa sare ya 1-1 nyumbani, bao la wenyeji likitiwa kimiani na Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, kabla ya wageni kuchomoa kipindi cha pili.
Wakati huo, Yanga ikifundishwa na Raoul Shungu kutoka DRC, kikosini ikiwa na wakali kama Manyika Peter, Ally Mayay, Said Mwamba ‘Kizota’ (marehemu), Sekilojo Chambua na Edibily Lunyamila, ilifungwa 4-0 katika marudiano.
Hata hivyo, siku hiyo kipa wa Yanga, Ismail Suma alitolewa nje kwa kadi nyekundu, timu hiyo ikiwa nyuma kwa bao 1-0 na mshambuliaji Said Mhando (marehemu) akaenda kusimama langoni, ndipo mvua ya mabao ikawamiminikia.
Lakini kwa ujumla Yanga haijawahi kuifunga timu yoyote ya Misri tangu ianze kukutana nazo mwaka 1982 kwenye michuano ya Afrika.
Mwaka 1982 katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa, Yanga ilifungwa 5-0 na Al- Ahly mjini Cairo, kabla ya kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
Mwaka 1988 Yanga ilifungwa 4-0 na Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa, baada ya awali kulazimishwa sare ya bila kufungana Dar es Salaam.
Mwaka 1992 Yanga ilitoa sare ya 1-1 na Ismailia mjini Cairo, bao lake likifungwa na Kenneth Pius Mkapa baada ya awali kufungwa 2-0 Dar es Salaam katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa.
Mwaka 2009 Yanga ilifungwa na Al Ahly 1-0 Dar es Salaam ikitoka kufungwa 3-0 mjini Cairo katika Ligi ya Mabingwa na mwaka 2000 ilifungwa jumla ya mabao 5-1 na Zamalek katika Kombe la Washindi.
Mwaka jana Yanga, ilicheza Kombe la Shirikisho na kutolewa Raundi ya Kwanza tu na Dedebit ya Ethiopia kwa kufungwa jumla ya mabao 6-4, ikitoa sare ya 4-4 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-0 Addis Ababa.
Mafanikio makubwa kwa Yanga katika michuano ya Afrika ni kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa 1998, na wakati michuano hiyo ikiitwa Klabu Bingwa Afrika, walicheza Robo Fainali mara mbili 1969 na 1970 na walifika pia Robo Fainali ya Kombe la Washindi mwaka 1996.
Katika mchezo wa kesho, hapana shaka kocha Kostadin Papic atamsimamisha langoni Mghana Yawe Berko, ambaye hajacheza hata mechi moja ya ligi mzyunguko huu wa pili, kwa sababu alikuwa mgonjwa ila amepona na yuko fiti.
Hata hivyo, Shaaban Kado amedaka vizuri mechi tatu za mzunguko wa pili kitu ambacho kwa upande mwingine kinaweza kuwa mtihani kwa Papic, ampange nani.
Nahodha Nsajigwa Shadrack anaweza kuanza beki ya kulia na kushoto Stefano Mwasyika wakati Athumani Iddi ‘Chuji’ atasimama katikati na Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ na kiungo mkabaji anaweza kuwa Juma Seif ‘Kijiko’.
Kiungo mchezeshaji haloina mjadala, ni Haruna Niyonzima na kulia hapana shaka atacheza Omega Seme, kushoto Hamisi Kiiza na washambuliaji watakuwa Kenneth Asamoah na Davies Mwape.
Bila shaka Papic ataendelea na desturi yake ya kumuinua Shamte Ally Kilalile kwenda kuongeza kasi ya mashambulizi kipindi cha pili, akimpokea Omega.
Rashid Gumbo, Jerry Tegete na Pius Kisambale wote wapo fiti na yeyote kati yao anaweza kuongeza kasi ya mchezo akiinuka kutokea benchi.
Katika mchezo huo, Yanga inatakiwa kucheza kwa umakini wa hakli ya juu, kwani Zamalek inaundwa na wachezaji wazoefu na uwezo mkubwa kama Amr Zaki, aliyewahi kucheza Ulaya.
Yanga wanatakiwa kuumiliki mpira kwa muda mrefu ili kuwazuia wapinzani wao, lakini wakithubutu kuwaachia Waarabu wakae nao mpira, wataumia.
***REKODI YA YANGA NA TIMU ZA MISRI***
MWAKA 1982: Ligi ya Mabingwa
RAUNDI YA PILI:
Al- Ahly (Misri) Vs Yanga 5-0: 1-1
MWAKA 1988: Ligi ya Mabingwa
RAUNDI YA KWANZA:
Yanga Vs Al-Ahly 0-0: 0-4
MWAKA 1992: Ligi ya Mabingwa
RAUNDI YA KWANZA:
Yanga Vs Ismailia 0-2: 1-1
MWAKA 2009: Ligi ya Mabingwa
RAUNDI YA KWANZA
Al Ahly Vs Yanga 3-0: 0-1
MWAKA 2000: Kombe la Washindi
RAUNDI YA KWANZA
Yanga Vs Zamalek (Misri) 1-1: 0-4

0 comments:
Post a Comment