// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WHITNEY HOUSTON AZIKWA KESHOKUTWA, HUENDI BILA MWALIKO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WHITNEY HOUSTON AZIKWA KESHOKUTWA, HUENDI BILA MWALIKO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 16, 2012

    WHITNEY HOUSTON AZIKWA KESHOKUTWA, HUENDI BILA MWALIKO

    LOS ANGELES, Marekani
    WHITNEY Houston anatarajia kuzikwa keshokutwa (Jumamosi) kwenye makaburi jirani na kanisa ambalo aliimba kwaya alipokuwa mdogo, mjini New Jersey, lakini watu wachache tu ndiyo watakaoshiriki mazishi yake tena kwa mwaliko maalum toka familia yake.
    Kwa mujibu wa taarifa toka sehemu atakayozikwa, 'Whigham Funeral Home', mazishi yake yatafanyika majira ya saa sita mchana, ambapo kabla itafanyika ibada kwenye kanisa la New Hope Baptist.
    Whitney, 48, alikutwa amekufa Jumamosi iliyopita kwenye bafu la hoteli ya Beverly Hills.Mwili wake ulisafirishwa kwenda mjini New Jersey na kupokelewa kwenye uwanja wa Ndege wa Teterboro Jumatatu wiki hii na kisha kupakiwa kwenye gari maalum ililopendezeshwa na madini ya dhahabu.
    Msimamizi wa makaburi hayo, Carolyn Whigham, alisema siyo watu wote watakaoruhusiwa kushiriki mazishi hayo ila kwa wale tu watakaopewa mwaliko maalum.
    "Amekuwa kwenye mji huu karibu miaka 30 akiimba, kwenye jimbo na duniani," alisema wakati akiongea na waandishi wa habari na kuongeza: "Sasa ni wakati wa wao pia kumuaga."
    Uchunguzi wa sababu za kifo chake ulifanyika Jumatatu, lakini itachukua zaidi ya wiki nane kabla ya kufahamu chanzo.
    Mpaka sasa hakuna kesi yoyote iliyofikishwa mbele ya vyombo vya sheria kuhusu kifo chake, Polisi wa Los Angeles walisema na kuongeza: "Chumbani kwake hakukuwa na maelezo ya matumizi ya dawa."
    "Houston alikutwa amekufa kwenye sinki la kuogea katika bafu la hoteli aliyofikia," taarifa zilisema.
    Rambirambi za maua na mishumaa zimewakwa nje ya kanisa alilokuwa akiimba alipokuwa mdogo katika mji mdogo wa Newark.
    "Baada ya kukutwa katika hali isiyoelewa, Whitney alipewa huduma ya kwanza, lakini muda mfupi baadaye ilijulikana kwamba alishafariki zamani," taarifa zilisema zaidi.
    Hata hivyo Polisi hawataki kuamini kama dawa zilizokutwa chumbani kwake zinaweza kuwa chanzo cha kifo chake.
    "Idara yetu ya uchunguzi wa Polisi Beverly Hills, haijajiridhisha kuamini uvumi unaoendelea kusemwa wakati huu kuhusu kifo chake," alisema Luteni Rosen. "Hatuna uthibitisho na uvumi huo."
    Lakini alikiri kwamba kulikuwa na chupa za dawa kwenye chumba cha Whitney
    "Zilikutwa chupa nyingi za dawa," alisema Ed Winter, msaidizi kanali.
    "Alikuwa shabiki wa kila mmoja," alisema Gregory Hanks, 26, mcheza filamu katika mji alikozaliwa Houston.
    Taarifa toka Ikulu ya Marekani, zinasema Rais Barack Obama ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WHITNEY HOUSTON AZIKWA KESHOKUTWA, HUENDI BILA MWALIKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top