KLABU inayomilikiwa na gwiji wa soka Ghana, Abedi 'Pele' Ayew, Nania FC imejitoa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho dakika za lala salama.
Sababu za Nania FC kujitoa kwenye michuano hiyo, ambayo Tanzania inawakilishwa na Simba Sc ni kujitoa kwa wadhamini wao wakuu, hali ambayo inawaacha buila fedha za kutosha za kushiriki michuano hiyo. Uamuzi wao umekuja siku mbili kabla ya kuikabili Sequence FC ya Guinea kwenye mechi ya kwanza, waliyopangiwa kuanzia nyumbani.
"Abedi anajisikia vibaya na hali hii, baada ya kukosa njia nyingine yoyote, klabu iliamua ni vema kujitoa,"alisema Msemaji wa klabu, Fiifi Tackie.
FC Nania inacheza Ligi Daraja la Pili Ghana, lakini walipata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho baada ya kutwaa Kombe la FA la Ghana mwaka jana, kwa ushindi wa dakika za nyongeza dhidi ya Asante Kotoko kwenye fainali.
0 comments:
Post a Comment