Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha soka (FAT) sasa (TFF),
Michael Wambura amewasilisha rasmi barua ya pingamizi dhidi ya mgombea wa
Uenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA), Amin Bakhressa.
Wambura amesema amewasilisha barua yake DRFA na kupokelewa
na mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi Kanuti Daudi alisema kwamba Katiba ya DRFA
ibara ya 29 (3) inamtaka mgombea kuwa na sifa zilizoainishwa kwenye ibara ya
30(2) ya elimu ya kidato cha nne, huku ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa
wanachama wa TFF inamtaka mgombea yeyoye lazima awe na elimu ya kidato cha nne
inayoambatana na cheti cha matokeo.
“Kwa mantikiti hiyo Amin Mohammed Salim (Bakhressa) anakosa
sifa ya kuwa mgombea Uenyekiti wa DRFA kwa kuwa hana elimu ya kidato cha nne
kinachoambatana na cheti cha matokeo, hivyo jina lake liondolewe
katika orodha ya wagombea waliopitishwa kugombea uongozi wa DRFA,”Alisema
Wambura.
Aidha, Wambura pia amewatolea pingamizi wapiga kura wa DRFA
Abeid Mziba (Kinondoni), Saleh Ndonga (Temeke) na Amar Balhaboo (Ilala) ambao nao wanadaiwa kutokuwa na elimu ya
kidato chga nne pamoja cheti cha matokeo.
“Naomba kamati itamke wazi kuwa viongozi hao walichaguliwa
kimakosa bila kuzingatia kanuni za uchaguzi za TFF hivyo nafasi zao zitangazwe
ziko wazi ili wapatikane watu wenye sifa
za kikanuni kugombea,”Aliongeza Wambura.
Uchanguzi wa DRFA umepangwa kufanyika Machi 18 katika sehemu
ambayo itatangazwa ambapo kamatyi ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake Alhaj
Muhidin Ndolanga imeshafanya usaili na kutanga majina ya wagombea wa nafasi
mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment