BONDIA Vitali Klitschko alifanikiwa kuhifadhi mkanda wake wa WBC uzani wa heavy mjini Munich, Ujerumani, licha ya kwamba mpinzani wake kutoka London, Dereck Chisora, alimtoa jasho hadi mwisho wa pigano hilo.
Chisora, ambaye amepungua kwa nchi sita akijilinganisha na kimo cha bondia huyo wa Ukraine, alionekana akiwa wa kwanza kushambulia katika kila raundi ya pigano hilo la raundi 12.
Klitschko, mwenye umri wa miaka 40, huenda sasa akataka kupigana tena na bingwa wa zamani kutoka Uingereza, David Haye.
Tangu kengele ya kwanza ilipolia, Chisora, ambaye ni mzaliwa Zimbabwe, alionyesha ukakamavu, akisonga mbele kumshambulia bingwa wa dunia na kujaribu kuvuruga mbinu za Klitschko za kujihami.Lakini bingwa huyo wa dunia ambaye hajawahi kupigwa katika mapambano 44 ya kulipwa, alionyesha ni stadi mno kwa kukwepa makonde ya Chisora, na mara kwa mara akimwangushia ngumi kali za kichwa kwa mkono wa kulia.
Pigano hilo lilikwisha kwa mabondia hao wawili kujibizana kwa matusi, huku mdogo wake Klitschko, Wladimir Klitschko akisimama kati yao.
Ushindi huo bila shaka ni funzo kwa Chisora ambaye alimuonyesha Klitschko ujeuri hata kabla ya pambano, wakati alipomzaba kofi siku ya Ijumaa wakati mabondia hao wawili wakipimwa uzani mbele ya waandishi wa habari.
Frank Warren, ambaye anapanga mapambano ya Chisora, sasa amesema anamtaka Muingereza huyo aidha kupigana tena na Klitschko, au angalau mdogo wake, Wladimir
0 comments:
Post a Comment