Christosiler Kalatachristosiler@yahoo.com
Sent:Wed 2/15/12 1:28 PM
Nikiwa mwanamichezo ninayeipenda nchi yangu na hasa hivi vilabu vyetu vikubwa Yanga na Simba nashindwa kuelewa hivi viingilio wanavipanga kwa lengo gani, kuvikosesha mapato makubwa au kunafanyika hujuma?
Nimesoma katika gazeti moja la michezo, viingilio vimepangwa, Tshs 50,000, 30,000, 20,000, 15,0000, 7,000, na 3,000. Kwa mahesabu ambayo hayahitaji mtu kwenda shule, uwanja una uwezo wa kuingiza watu 60,000 kwa kiwango cha hapo juu maana yake sio wote watakao ingia.
Na kama watu 30,000 wataingia kwa kulipa Tshs 50,000, 30,000, 20,000 maana yake zitapatikana Tshs Bilioni 1.0 Je hilo linawezekana kweli ?
Haya tuje wale 30,000 waliobaki tunatazamia wataingiza Tshs 250,000,000.
Kwa takwimu hizi ina maana zitakusanywa Tshs Bilioni 1.25 hivi inawezekana kweli, na tujiulize imewahi kutokea ?
Nashauri vilabu hivi vikubwa na viongozi wa TFF wawe na Mchumi, kila kitu kinahitaji utaalamu sio kwenda kama vipofu hatutafika mbali mwishoni tutazidi kuwa maskini na tegemezi na kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe.
Nashauri viingilio viwe 30,000, 20,000, 10,000 na 7,000, 5,000, 3,000 na kwa hakika mapato yatakuwa Tshs 600,000,000.na Tshs 150,000,000.Jumla zinaweza kupatikana Tshs 750,000,000.
Huu ni mtazamo wangu, ukichukuliwa kwa umakini na kurekebishwa kidogo, Yanga wanaweza kutoka hata na Tshs 800,000,000.Naomba ujumbe huu uchapwe gazetini na tuone mapato yatakayo patikana J-mamosi kama yatakuwa namna gani. Mdau wa Mpira.
Mtanzania Halisi.
0 comments:
Post a Comment