Mkoa unaotaka kuwa mwenyeji wa fainali za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoshirikisha timu tisa bora za ligi hiyo unatakiwa kutoa sh. milioni 25 ambazo ni gharama za kuendesha fainali hizo.
Haki ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo iko wazi kwa mikoa yote wanachama wa TFF ingawa tayari ipo minne ambayo imeshatuma rasmi maombi ya kuandaa fainali hizo. Mikoa hiyo ni Mbeya, Mwanza, Ruvuma na Tabora.Kwa mikoa ambayo itakuwa tayari kuwa mwenyeji kwa maana ya kutimiza sharti hilo la kutoa kiasi hicho cha fedha inatakiwa iwe imefanya hivyo kufikia Machi 15 mwaka huu.
Pia kumefanyika mabadiliko ya kuanza fainali hizo, sasa zitaanza Machi 31 mwaka huu badala ya Machi 17 ambayo ilitangazwa awali.
0 comments:
Post a Comment