Machi
8 kila mwaka ni Siku ya Wanawake Dunia. Ili kuadhimisha siku hiyo kwa
upande wa mpira wa miguu, TFF kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa
Miguu cha Wanawake (TWFA) imeandaa mashindano mafupi kwa shule nane za
sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam.
Mashindano
yataanza Februari 24 mwaka huu kwenye viwanja viwili vya Jitegemee
Sekondari ambapo kutakuwa na kundi B wakati kundi A litacheza mechi zake
Makongo Sekondari. Mechi zitaanza saa 8 mchana na kumalizika saa 10
jioni.
Kundi A lina shule za Makongo, Goba, Twiga na Lord Barden wakati Jitegemee, Benjamin Mkapa, Kibasila na Tiravi zitakuwa kundi B.
Lengo
la mashindano ni kuhamasisha mpira wa miguu kwa wasichana katika ngazi
ya shule, kuandaa, kubaini na kuendeleza mafanikio yanayopatikana katika
timu ya wanawake ya Taifa.
Pia
kutoa fursa kwa watoto wa kike kusherehekea Siku ya Wanawake duniani
kupitia mpira wa miguu, kutekeleza ushiriki wa TFF katika shughuli za
kijamii na ni sehemu ya mchakato wa kuandaa mashindano ya ligi kwa
wasichana.
Uchaguzi
wa timu shiriki umezingatia mchango wa shule katika kuendeleza mpira wa
miguu kwa wasichana/wanawake. Pia zawadi zitatolewa kwa mshindi wa
kwanza, pili na tatu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo ni Zainab Mbiro kutoka Twiga
Sekondari wakati wajumbe ni Brighton Mbasha (Jitegemee),
Yusuf Mohamed (Tiravi), Michael Bundala (TFF), Furaha Francis
(TFF/TWFA) na Rose Kissiwa (TWFA).
Tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kusaidia gharama za uendeshaji wa mashindano hayo.
FAINALI FDL KUANZA MACHI 17
Hatua ya fainali ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) itafanyika kuanzia Machi 17 mwaka huu katika kituo ambacho kitatangazwa baadaye.
Timu
tatu kutoka katika kila kundi ndizo zitakazocheza fainali hiyo.
Washindi watatu wa juu ndiyo watakaofuzu kucheza Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) msimu ujao.
Mikoa
mitatu ya Mbeya, Mwanza na Ruvuma imewasilisha maombi ya kuwa wenyeji
wa fainali hizo. Maombi hayo yanafanyiwa uchambuzi kabla ya kutangaza
mkoa uliopewa nafasi hiyo.
Wakati
huo huo, michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) hatua ya makundi
inamalizika kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tatu za kundi A.
Polisi
Dar es Salaam watakuwa wenyeji wa Morani FC ya mkoani Manyara katika
mechi itakayochezwa Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Mgambo
Shooting Stars ya Tanga itaoneshana kazi na Temeke United ya Dar es
Salaam katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
wakati Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro utashuhudia mechi kati ya
wenyeji Burkina Faso na Transit Camp ya Dar es Salaam.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment