Carlos Tevez ameichezea Manchester City kwa mara ya kwanza tangu arejee baada ya kuigomea kwa miezi kadhaa.
Tevez alicheza nusu ya kwanza katika mchuano maalum wa timu za wachezaji akiba kati ya Man.City na Preston.Ulikuwa ni mchuano wa faragha katika viwanja vya ndani, lakini Tevez hakuweza kufunga bao na Preston waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo Tevez alishiriki vilivyo katika mchezo.
Tevez alikorofishana na kocha Roberto Mancini baada ya kushtumiwa kwamba alikataa kufanya mazoezi wakati Chelsea iliposhindwa na Bayern Munich mwezi Septemba.
Baadae Tevez alikaa zaidi ya miezi mitatu nchini Argentina bila ya idhini ya klabu hiyo.
Alirejea Uingereza wiki mbili tu zilizopita baada ya kushindwa kupata uhamisho kwenda klabu yoyote wakati wa dirisha la Januari na kuomba msamaha kwa Mancini.
0 comments:
Post a Comment