// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SOKA YETU YAZIDI KUPOROMOKA MASIKINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SOKA YETU YAZIDI KUPOROMOKA MASIKINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 16, 2012

    SOKA YETU YAZIDI KUPOROMOKA MASIKINI

    TANZANIA imeporomoka kwa nafasi mbili kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka Ulimwengu (Fifa), huku mabingwa wapya wa Afrika, Zambia pamoja na Equatorial Guinea na Gabon zikipanda juu kwa kasi ya ajabu.
    Tanzania iliyokuwa ikishika nafasi ya 137 mwezi uliopita sasa imeporomoka hadi nafasi ya 139 kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
    Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati katika Kombe la Chalenji, Uganda wanaongoza kwa ubora kwa kushika nafasi 87, nayo Sudan iliyofuzu kwa robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika ipo nafasi ya 111.
    Kenya wanashika nafasi ya 123, Rwanda wapo nafasi ya 108, huku Burundi (143) na Ethiopia (137) .
    Wapinzani wa Tanzania katika kampeni za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013, Msumbiji wenyewe wanashika nafasi ya 102.
    Kwa mara ya kwanza tangu Februari 2001, timu inayofundishwa na kocha Herve Renard, imefanikiwa kuingia kwenye 50 bora baada ya Zambia kushika nafasi ya 43 katika orodha hiyo ya Fifa.
    Pamoja na kufungwa kwa penalti, Ivory Coast imepanda kwa nafasi tatu hadi 15 na kuongoza kwa ubora kwa timu za Afrika. Nayo Mali iliyoshika nafasi ya tatu imepanda juu kwa nafasi 25 hadi kufikia kuwa ya (44, huku wenyeji wenza wa fainali hizo za Afrika Gabon ipo nafasi ya 45 kwa kupanda juu kwa nafasi 46 na Equatorial Guinea wakipaa kwa nafasi 41 hadi 110 .
    Mabadiliko pia yamejitokeza kwenye timu 10-bora kwa Ujerumani kuishusha Uholanzi kwenye nafasi ya pili na kuisogelea Hispania kileleni, Ureno imepanda kwa nafasi moja hadi namba sita na pia imejisogeza nafasi ya nane. Denmark imeingia kwenye 10-bora na kuiporomosha Argentina hadi nafasi ya 11.
    Mabadiliko hayo yote ya viwango vya ubora wa Fifa inatokana na timu nyingi kutocheza mechi katika mwezi uliopita.
    Ubora wa viwango kutoka kwenye mashirikisho umebaki vilevile: UEFA imeingiza timu 27 kwenye 50 (moja ikitoka nje), CONMEBOL imeingiza tisa, CAF sita, CONCACAF nne na AFC pia nne wakati OFC haina timu. Orodha nyingine ya ubora wa viwango ya Fifa inategemewa kutolewa Machi 7 2012
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SOKA YETU YAZIDI KUPOROMOKA MASIKINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top